Sunday, November 11, 2012

Questions

Mwambu, Salome Daudi  [CCM]
Iramba Mashariki Constituency
Session No Question No To the Ministry of Sector Date Asked
5 7 AGRICULTURE, FOOD SECURITY AND CO-OPERATIVES Food/Agriculture 8 November 2011
Principal Question No
Mkoa wa Singida hususan Wilaya ya Iramba Mashariki ilipewa vocha chache za majaribio tu na kwa zao la mtama pekee wakati mazao kama mahindi na alizeti nayo yanastawi vizuri:

(a) Je, Mkoa wa Singida utaondolewa lini kwenye majaribio na kupatiwa vocha za kutosha kwa mazao yote?

(b) Je, ni lini Serikali itatambua kuwa mazao mengine kama mahindi na alizeti yanastawi vizuri na yanastahili pembejeo pia?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #7 SESSION # 5
Answer From Hon. Chiza, Eng. Christopher Kajoro
AGRICULTURE, FOOD SECURITY AND CO-OPERATIVES
NAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Salome Daudi Mwambu, Mbunge wa Iramba Mashariki, lenye sehemu (a) na (b) yote kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Singida kama ilivyo kwa mikoa mingine unashirikishwa moja kwa moja katika mpango wa ruzuku katika mbolea na mbegu bora za mazao ya chakula hususan mahindi na mpunga kwa kutumia utaratibu wa vocha. Aidha, ruzuku pia hutolewa nje ya utaratibu wa vocha kwa mbegu za alizeti na mtama. Hata hivyo takwimu zinaonesha kwamba matumizi ya pembejeo katika Mkoa wa Singida bado yapo chini sana. Kwa mfano, katika msimu wa mwaka 2010/2011, Mkoa ulipokea vocha zenye thamani ya shilingi 1,725,245,000 na kutumia vocha zenye thamani ya shilingi 1,465,344,500 sawa na asilimia 85 ya thamani ya mapokezi asilimia 15 zilirudishwa.

Katika msimu huo pembejeo zilizopelekwa Mkoani Singida ni tani 2573.10 za mbolea, tani 200 za mbegu ya mahindi na tani 85.97 za mbegu ya mpunga. Aidha, Mkoa ulipokea tani kumi za mbegu ya alizeti yenye ruzuku. Katika mwaka 2011/2012 Mkoa wa Singida umetengewa tani 2573.10 za mbolea, tani 220 za mbegu ya mahindi, tani 37.31 za mbegu ya mpunga kwa utaratibu wa vocha. Aidha, nje ya utaratibu wa vocha, Mkoa huo pia utapata tani 20 za mbegu ya alizeti na tani 40 za mtama zenye ruzuku.

0 comments:

Post a Comment