Sunday, November 11, 2012

Questions

Mwambu, Salome Daudi  [CCM]
Iramba Mashariki Constituency
Session No Question No To the Ministry of Sector Date Asked
7 99 PRESIDENT'S OFFICE (PUBLIC SERVICE MANAGEMENT) Employment 19 April 2012
Principal Question No
Serikali imeazimia kujenga Vituo vya Afya kwa kila kijiji na shule za
sekondari kwa kila Kata, hata hivyo shule za Kata hazina walimu wala
vifaa vya kufundishia na pia zahanati zetu hazina watumishi wa kutosha
na kwamba miaka ya nyuma Serikali iliazimia kuwaajiri kwa mkataba
maalum watumishi wa Elimu na Afya waliostaafu lakini zoezi hilo
likasitishwa.

Je, Serikali itarudisha lini ajira hizo za mkataba kwa kada hizo zenye
upungufu mkubwa wa watumishi?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #99 SESSION # 7
Answer From Hon. Ghasia, Hawa Abdulrahman
PRESIDENT'S OFFICE (PUBLIC SERVICE MANAGEMENT)
WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Salome
Daudi Mwambu, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, utaratibu wa kuwaajiri watumishi kwa mikataba
umeanisha katika Kanuni D. 28 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa
Umma toleo la 2009 na waraka wa Rais, Na. 1 wa mwaka 1998.

Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo haya ajira za mikataba
hasa katika maeneo yenye mahitaji makubwa kama vile Afya na Elimu
zitaendelea kutolewa kwa mujibu wa Kanuni nilizozitaja.

0 comments:

Post a Comment