Sunday, November 11, 2012

Questions

Mwambu, Salome Daudi  [CCM]
Iramba Mashariki Constituency
Session No Question No To the Ministry of Sector Date Asked
8 222 FINANCE AND ECONOMIC AFFAIRS Pension 18 July 2012
Principal Question No
Kuanzia mwaka 2005 Wastaafu wanalipwa kwa
mkupuo wa miezi sita sita na pensheni yao ya miaka
mitatu na kwamba hulazimika kufuata mlolongo mrefu
wa kujaza fomu na kuzifuatilia Dar es Salaam.

(a) Kwanini Serikali imeweka tofauti katika kulipa mafao?

(b) Je, ni lini Serikali itaondoa mlolongo mrefu wa kusogeza shughuli hizo mikoani?

(c) Je, ni lini Serikali itatambua kuwa kiwango wanacholipwa wastaafu kimepitwa na wakati na hivyo kufanya marekebisho?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #222 SESSION # 8
Answer From Hon. Salum, Saada Mkuya
FINANCE AND ECONOMIC AFFAIRS
NAIBU WAZIRI alijibu:-

Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha
napenda kujibu swali la Mheshimiwa Salome D.
Mwambu, Mbunge wa Iramba Mashariki, lenye
sehemu (a), (b) na ( c) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, Serikali inawalipa wastaafu
pensheni zao kupitia akaunti binafsi za wastaafu hao kwa vipindi vya miezi mitatu mitatau kuanzia Januari mwaka 2012 kama Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
inavyolipa.

Asilimia 20 ya mchango wa mwanachama
inatumiwa na mifuko yote. Hakuna tofauti ya muda
uliopo katika kuwalipa pensheni wastaafu isipokuwa
kuna tofauti ya vigezo (package factors) vya
kukokotoa mafao kati ya Serikali na Mifuko mingine
kama NSSF na PPF. Aidha, Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (Social Security Regulatory Authority (SSRA) kwa kushirikiana na Benki Kuu imefanya tathmini ya kuangalia namna ambavyo kila mfuko utatumia kikokotoa linganishi na mfuko mwingine katika kutoa mafao kwa Wastaafu bila kuathiri ukuaji wa mifuko.

Matokeo ya tathmini hii yatawasilishwa kwa
wadau wa masuala ya pensheni siku ya Ijumaa tarehe
20 Julai, 2012 kwa ajili ya kujadiliwa na kupokea
mapendekezo kwa ajili ya hatua za kuandaa Waraka
kwenda Baraza la Mawaziri kwa ajili ya idhini. Hivyo, ni imani ya Serikali kuwa suala la kutumia vikokotoa vipya na linganishi kwa mifuko yote ya pensheni litakamilika mapema na kuanza kutumika na wadau wote wa pensheni.

(b) Mheshimiwa Spika, utaratibu wa kuzitumia
Hazina Ndogo kuratibu huduma za pensheni kwa kila
Mkoa na kulipa pensheni zao kupitia akaunti zao za
benki unawawezesha wastaafu kupata pensheni zao
huko huko walipo na hivyo sisi Serikali tunadhani
utaratibu huu bado unakidhi mahitaji ya wastaafu.

(c) Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kuwa
kiwango cha pensheni wanacholipwa wastaafu
hakikidhi mahitaji yote ya lazima. Serikali imekuwa ikiongeza kiwango cha pensheni pale ambapo uwezo wa kufanya hivyo unaruhusu. Kwa mara ya mwisho Serikali iliongeza kiwango cha chini cha pensheni kutoka shilingi 21, 601/= kwa mwezi hadi shilingi 50,114/= kwa mwezi Julai, 2009. kiwango cha shilingi 21,601/= kilianza kutumia kuanzia Julai, 2004 hadi Juni mwaka, 2009. Serikali itaangalia uwezo wake wa kumuda ongezeko la kima cha chini cha pensheni na itakapoona uwezo upo na ni endelevu haitasita kuongeza pensheni hizo.

0 comments:

Post a Comment