Saturday, July 25, 2015

nimebahatika "kupata" mahala ka-Mtaji. Ni kiasi cha shs. milioni kumi tu, (10,000,000/=) za Kitanzania.

Nipeni mapendekezo nizi invest wapi, kivipi na matarajio ya faida.
(i.e biashara gani inalipa (plus location), kwa muda gani, na SWOT analysis zake)

                            MAPENDEKEZO
Quote By Mgombezi View Post
Mimi ni mfugaji, nitakushauri kufuga ngombe kwa mchakato ufuatao:

Ujenzi wa banda = Ths 500,000/=
Manunuzi ya Ngombe 5 x Tsh 900,000 = Tsh 4,500,000/=
(Ng'ombe utawanunua wakiwa na mimba ya miezi 6)
Kuwahudumia ng'ombe kwa miezi mitatu kabla ya production = Tsh 1,500,000/=
(inahusisha mshahara kwa wafanyakazi wawil + chakula + madawa)

Jumla = Tsh 6,500,000/=

Baada ya Miezi 3;

UZALISHAJI:

Ngombe hawa watakuwa wakitoa maziwa si pungufu ya lita 5 kwa asubuhi na jioni kwa kila ng'ombe. Hivyo uzalishaji kwa siku utakuwa lita 10 kwa siku kwa ng'ombe.

MAPATO

Lita 10 x Ng'ombe 5 = lita 50 kwa siku x Tsh 1000 (bei ninayouza mimi hapa) = Tsh 50,000 kwa siku
Mapato kwa mwezi = Tsh 50,000 x 30 = 1,500,000/=

Gharama za uendeshaji kwa mwezi = Tsh 600,000/=

Faida = Tsh 900,000/= kwa mwezi

BAADA YA MIAKA 5:

Kumbuka ng'ombe huzaa kila mwaka hivyo basi baada ya miaka mitano utakuwa na ng'ombe wasiopungua 25. Kipato chako kwa mwezi unaweza kufikia si pungufu Tsh 18,000,000 endapo utakuwa na ngombe jike 20 kati ya hao 25.

Quote By Malila View Post
kama una umri kati ya miaka 25 mpaka 35 nakushauri wekeza ktk misitu ya miti ya mbao(exortic) na nguzo za umeme,biashara ya nguzo za umeme kwa sasa inalipa ile mbaya,investment ktk misitu ya nguzo unafanya bila taabu hata kama uko Ulaya. Only risk takers can do it. Tz ardhi ni cheap sana.

Pili Ng`ombe safi pia. Tatizo la kuku wa kienyeji wafugaji wadogo wadogo wengi mno si rahisi kupredict soko la uhakika.Tatu jaribu kufuga samaki,tilapia au nile perch,wanazaliana kwa kasi na soko lake ni kubwa sana kwa sasa.
Kwa ufupi nimekuwa ktk sector hii ya miti kwa muda mrefu sana. Naomba mchague wenyewe eneo mnalotaka nishushe data kati zifuatazo;

1; Ardhi ya bei poa iko wapi? na taabu za huko
2; mbegu zinapatikana wapi? na namna ya kuotesha?
3; Aina ya mti(mbegu,growth rate,soko,na sehemu ya kupanda ktk Tz)
4; Msimu mzuri na maandalizi yake.
5; overhead cost baada ya kupanda.
6; Field management.

Leo niwape item ya tatu tu,mimi nimeajiriwa,najaribu kutumia muda wa mwajiri kwa uangalifu.
Kuna miti mingi ila kwa sisi mizuri ni hii; mitiki(10, nje),milingoti boriti(8),milingoti nguzo (10), milingoti mbao (15),mikrismas(cyprus mbao) (25),
pines (12),ktk mabano ni miaka toka kupanda mpaka kuvuna. Soko la mitiki liko nje ya nchi,locally hakuna commercial market mpaka Kilombero wakijenga kiwanda mwakani. Mbegu zinapatikana kwa wakala wa serikali Morogoro,Iringa,Arusha,Tanga etc. Mbegu za mitiki ni ngarambe kuotesha, kilo moja ni Tsh 6000/ na ukifuata utaalam unapata miche 1000 hivi,lakini wajanja wanafanya kienyeji na wanapata zaidi au wanatumia suckers fulani hivi. Bei ya mche kwa sasa ni Tsh 500/ ya chini na 2000/ ya juu pale dar.

Pine/cyprus kilo moja ni Tsh 18,500/ na unapata miche 30,000 mpaka 35,000 inatosha eka hamsini ya miti ya mbao. Mlingoti kilo moja ni Tsh 22,500/ na unapata miche 120,000. Unapanda boriti eka 100 na unapanda miti ya mbao eka 200.

Utamu uko ktk boriti. Eka moja ni boriti 1200,bei ya boriti moja kwa leo hii ni Tsh 15,000/shambani.kwa hiyo eka moja iliyogharimu Tsh 70,000/ kununua ardhi mpaka kupanda itakupa 1200 x 15,000/=( ) toa gharama za fire break mara moja kwa mwaka. Hakuna kupalilia wala kumwagilia.

Mitiki peke yake inakubali pwani,mingine yote ni ktk nchi za baridi. Nimetoa kwa ufupi sana, ila tutaendelea kuelezana kidogo kidogo,
Mradi mwingine mzuri wa bei nafuu ni mradi wa kukamua alizeti. Mwaka jana nilipata bahati ya kutembelea Singida. Nikapata muda nikaenda mitaa ya sido. Nilitembelea viwanda vidogo vya kukamulia alizeti. Nikatafiti gharama za mradi wote ule. Kwa mujibu wa Sido,mtambo wenyewe unafikia Tsh 6,000,000/ kwa mwaka jana. Ila mitambo ya mitaani inaweza kuwa chini ya hapo. Gharama za jengo zinategemea sehemu.Ukiweza kufunga kimtambo hicho,mikopo ya upanuzi toka Sido ni mingi bila urasimu.

Wale jamaa wanatengeneza hela sio mchezo. Nimegundua pia kuwa watu wanarudi ktk matumizi ya mafuta ya nafaka sana na ukulima wa alizeti/ufuta unaongezeka sana.

Quote By Kashaija View Post
Jenga Choo ya kulipia eneo la Kariakoo. Utakuwa na uhakika wa kurejesha gharama zako ndani ya muda mfupi kama ifuatavyo:

Wateja - Akina mama (200 * 100/= * 30days) = 600,000/=
- Akina baba (150 * 100/= * 30days) = 450,000/=
- Watoto/vijana/wanafunzi (200 * 100/= * 30days) = 600,000/=
JUMLA KWA MWEZI 1,650,000/=

Kwa mwaka (19,800,000), kwa miaka kumi (198,800,000/=).

Yaani baada ya miaka kumi utakuwa millionea mkubwa sana, na usisahau kurudi hapa BAHARI YA MAARIFA na kutushukuru.

NB: Kumbuka, uzuri mmoja kwa biashara hii, haina suala la mvua wala kiangazi. Kila siku biashara inaenda.

Quote By Bavuvi View Post
Kwa Tanzania Mil. 10 unaweza kupata faida ya mwaka kama ifuatavyo:

1. ukanunua used Corola na kuifanya taxi. Mradi huu unakuhakikishia a minimum net revenue ya Shs 2.92 mil per year (8000*365).
2. Hisa za TCC: 10mil. * 10% = 1 mil per year + annual appreciatiatin ya ?%
3. Gunia za mahindi June na kuuza December: 10 mil * 50% = 5mil
4. Ziweke deposit bank upate interest: 10 mil * 7% = laki 7
5. Anzisha ka-saccos kasiko rasmi (zikopeshe at interest): 10 mil * 17% = 1.7 mil
6. Nunua shamba, chimba kisima ufanye kilimo cha umwagiliaji: 10 mil * 2mil
7. NAENDELEA KUBUNGABONGO. WILL GET BACK TO YOU SHORTLY

Quote By Chiwa View Post
Tafuta eneo kama ekari mbili mpaka nne chimba kisima kama ulivyoelekezwa na ikiwezekana tenganisha matumizi ya maji binafsi na maji ya biashara. uza maji kwa ajili ya kutafuta gharama za kuendeleza na kukuza mtaji zaidi, lakini ni vizuri ukafuga kuku wa mayai kama 700 ambao nauhakika hutakosa tray 25 kwa siku kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, tumia fuga ngombe wa maziwa wawili tu watunze vizuri wakupatie lita 20-30 kwa siku, hata kama mazima haya lipi unahitaji mbolea kwa ajiri ya mbogamboga na kupata bio gas pamoja na matunda achilia mbali kwa sababu maji unayo unaweza kuwa na bwawa dogo la samaki ukaanza kuvuna kila miezi minne mara baada ya kupanga na haya chini ndio mapato kwa miezi sita kwa kila mwezi.

maziwa1,080,000.00
mbogamboga600,000.00
mayai4,500,000.00
maji450,000.00
samaki500,000.00
passion400,000.00
jumla7,530,000.00

Natengeneza mchanganuo ukikamilika nitwawasilisha kwenu, vinginevyo humu ndani kuna vibiashara na mawazo ya watu wengi nayaheshimu sana na yamenisaidia sana.

Kama muoga unaweza ukanunua ardhi kiasi wakati unajipanga.

Quote By Felix View Post
Wazo linguine la nyongeza mkuu ni hili, uko nje ulipo, angalia yafuatayo,

1.viwanda vya kutengeneza vyakula vya kuku-kama wanaweza kununua dagaa kutoka Tanzania.
2.Viwanda vyakutengeneza vyakula vya mifugo, na dawa za viatu kama kiw-ulizia kama wanaweza kununua mashudu ya alizeti kutoka tanzania
3. Viwanda vya kutengeneza viatu, mikoba, mikanda n.k- ulizia kama unaweza kuwa uzia ngozi za wanyama kama ngombe.
4. Viwanda vya kutengeneza taa za umeme, balb- ulizia kama wanaweza kununua kwato na pembe za ngombe.

Ukisha pata soko lake la uhakika, rudi jamvini kuomba watu wa kushirikiana nao ili kuongeza mtaji.bidhaa zote nilizo eleza kwa apa Tanzania zinapatikana sana. hivyo ukiomba watu wa kushirikiana nao uenda ukawapata na mimi naweza kuwa mmoja wapo kwa kuongeza zingine 10milion. na hivyo ukapeleka hata kwa kuanzia angalau contena moja.

ndo hayo tu mkuu. ubarikiwe

Quote By Bravo Engliash View Post
Mdau rasomaka;

Angalia mazingira unayoish, km inawezekana anzisha biashara ya bodaboda za mkataba (miez 10 baada ya hapo inakuwa ya kwake huyo dereva, matengenezo n jukumu la dereva)

Kwa 10 millions unanunua pkpk 4 (pkpk moja inauzwa around 1.8 mil san lg inapendwa zaid, ingawa zpo nyngne za bei pungufu)

Na kila pkpk kwa siku inaingza sh. elfu 10, baada miez 6 kila pkpk imeshajrudshia hela yake ya manunuz ile miez mi4 ilyobak faida. (Mwisho wa mkataba kila pkpk inazaa nyingine)

Biashara n kupata faida, kutanuka na kuzaa biashara nyingne.

Ukikusanya hela ya pkpk 4 kwa miez 3 (1,200,000×3=3600,000/=) ni hela ambayo unaweza kununua pkpk ya matairi matatu (bajaji) ya mizigo/maji ambayo itakuletea kipande kwa siku sh. elfu 15 ( kwa mwez lak 4 ukiondoa matengenezo)

Au kuamua kununua pkpk nyngne tena na kupanua wigo mkubwa wa bzness ambapo mpk pkpk za kwanza znaisha mkataba wake, ztakuwa zmeshazalisha nyngne nyingi.

Pia kwa hela unayokusanya unaweza kubuni biashara nyngne kutokana na eneo unaloish.

Changamoto:
Kila biashara haikosi changamoto, kwa pkpk changamoto kubwa ni kuibiwa/kutoroka na pkpk.

Mkataba uwe wa maandishi kwa m/kt wa mtaa ikiwezeka hata polisi mnaandkshiana ili kuwe na usalama.

Bodaboda ya mkataba n nzur kwa wote, tajiri na dereva, dereva anafaidika kwa kuwa baada ya kumalza mkataba anaimiliki inakuwa yake hivyo atakuwa makini na ataitunza. Matengenezo n jukumu lake.

Bodaboda za kipande kwa kila siku n majanga sana, dereva akishaona imechoka anaiacha na kutafuta nyingne mpya.

Ni hayo mawazo yangu nawasilisha.
Quote By Aiman Ayoub Mangi View Post
Kanunue hisa za crdb ambazo zinauzwa at shs 150 per share. 10 m itakupatia shares 66,666. Hii maana yake nini. 

ukinunua shares hizi crdb zikipelekwa kwenye soko la hisa unaweza ukaziuza zote halafu ukavuna zaidi ya asimia 100. Na hii ni baada sana sana ya miezi miwili.

Kwa hiyo ukipata 20m zako iko mbaya gani/ U can decide kuziweka kwenye Fixed deposit ya hao crdb halafu ukaitumia hiyo kuombea mkopo. But this depends very much if u have a steady monthly income. 

Huo ni ushauri wangu wa bure

Quote By Baba Ubaya View Post
Bandugu,

You will fail 100% kama utatumia approach ya kusikia kwa watu ndio utekeleze.

The best project must come from you and not from other people. Sisi wengine ni kukupatia minofu michache lakini you must have the skeleton.

Ndio hayo tu.

Quote By Mama Kilaree View Post
Mie naona Mbu uwekeze kwenye mfumo wa maji safi kule bongo, nenda sehemu ambazo hawana maji ya bomba na ukachimbe visima vya kutumia mota ya umeme ili wapate maji safi badala ya kuchota maji kwenye madimbwi. Hiyo pesa unaweza kuchimba visima 5, hapo utasaidia wananchi wenzako. Unaweza kurudisha pesa yako, iwapo utafanya kila ndoo ya maji ni shs 100.

Quote By malila View Post
je unataka investment ya muda mfupi au mrefu, specify,pili biashara hiyo utasimamia mwenyewe au unataka uweke mtu wa kuisimamia? Je unataka biashara hiyo ndo uitegemee kwa maisha ya kila siku? Uko tayari kwenda kinyume cha imani yako(kama una imani/dini) ?
...malila, nikikurudishia hili swali, Investment ipi ina faida zaidi, ya muda mfupi au muda mrefu? Halafu ukisema Investment ya muda mfupi/mrefu una maanisha nini? 

Kwa mfano; Biashara ya mama Ntilie, chapati na maandazo maofisini unaziweka kwenye kundi la short/long term investment? Kuhusu usimamizi na utegemezi inategemeana na ushauri nasaha toka kwenu wajasiriamali wazoefu.

Haya ndugu zangu mnaweza kuongezea mapendekezo yenu kwenye sehemu ya comments
Imeandaliwa na:
AYOUB MANGI,
Mtendaji mkuu,
BAHARI YA MAARIFA
whatsapp: 0755630055
Dar Es Salaam ,TANZANIA

5 comments:

  1. ATTENTION ATTENTION ATTENTION

    Mimi ni Mheshimiwa Smith Jones Alpha Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni binafsi mkopo, sisi kutoa mkopo kwa kiwango cha chini sana maslahi ya 1.5%. kama una kukataliwa na makampuni mengine mkopo, taasisi za fedha, Benki, kuangalia tena sisi ni hapa kukusaidia kutatua tatizo hilo yako haraka. sisi kutoa kila aina ya mikopo kama vile mikopo elimu, mikopo ya biashara, mkopo nyumbani, Kilimo mkopo, mkopo kibinafsi, Auto mikopo na sababu nyingine nzuri, kama vile ukitaka kuanzisha biashara, kampuni yetu inaweza kusaidia kwa mkopo. Sisi pia kutoa mikopo kutoka 5,000 - 2,000,000,000.Ruble, Dinar, Dola, Euro, na paundi, kwa kiwango cha 1.5%. Muda wa miaka 1- 50 kutegemea na kiasi unahitaji kama mkopo na wakati unahitaji kulipa nyuma. mkopo wetu imara ni kuwa nyuma na kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa, kwamba ni kwa nini sisi tu kupata 1.5% kama kiwango cha maslahi yetu si kama taasisi nyingine za fedha kwamba anapata 2%, 3% au hata 5% kutoka clients.Get yao nyuma na sisi kwa habari zaidi kupitia barua pepe yetu: smithjonesloanfirm@gmail.com.

    Regards, MR SMITH ALPHA JONES.

    ReplyDelete
  2. Chukua mil2 kachukue viazi mbeya. Gunia moja elf25 kutoka shamba hadi mjini cost inaweza fika elf35. Bei ya rejareja 55 hadi 45 faida inaweza kuwa15 hadi 20 kila gunia piga hesabu umechukua gunia 40×20,000=800,000 hiyo ndo faida ndani ya wiki. Kwa mwezi ukienda Trip 2×800,000=1,600,000

    ReplyDelete
  3. Ndugu mm nimewahi kufanya biashara nikiwa kijana mdogo Kama miaka kum na nane hivi nilikua nauza mbao na nilipata jina sana ila mtaji wangu ulikua ni mdogo na nilikua nakopa kwa watu waliokua wanaamin kazi yangu ninayo fanya lakin nilikuja nikafilisika mpaka kuishiwa kabisa nakarud tena kukopa bado nikaanguka tena ilikua ni biashara ya mbao japo nilikua na wateja wengi lakin bado nilianguka ikabid niache hiyo biashara nikafanya mishe zingine za kupasua tuu mbao coz na mashine za kuchania ila sasa nata kurud tena tena nikiwa na mtaji usio pungua mil 5 na mashine juu nifanyeje nisi filisike tena Bali nikuze mtaji wangu ufike kununua mbao Kama semi inavyo beba mtaji wa kuanzia ninao na sio mkopo ndug nishaur maana hii kazi naipenda na faida yake naijua maana na miaka tisa saiv

    ReplyDelete
  4. Naomba Kama utaona comment yangu basi utanishauri asante

    ReplyDelete