Tujifunze mbinu za kukopa fedha benki

NI wiki nyingine tena twamshukuru Mungu wetu kutujalia uhai. Awali ya yote kumekuwa na manung’uniko mengi kutoka kwa wajasiriamali dhidi ya mikopo ya benki, aidha ukiomba hupati kabisa au kiasi unachoomba kinapunguzwa na kuharibu malengo na au kuchukua muda mrefu muhusika kupata  mkopo.

Kimsingi benki na wajasiriamali wanategemeana sana. Ustawi wa benki hutokana na shughuli za ujasiraiamali wa ngazi zote; mdogo, wa kati na mkubwa.
Mjasiriamali anapaswa kukopa benki iweje wewe mwenye biashara ya kawaida usikope benki kama kampuni kubwa zinakopa kwa ajili ya kendesha shughuli zao!.
Suala la kukopa benki, linahitaji maandalizi ya kutosha na siyo kukurupuka tu kwani  unaweza kujikuta unaingia katika manung’uniko kama yalivyotajwa hapo awali. Benki zote duniani zina lengo la kumkwamua mjasiriamali katika ngazi zote.
Sasa ili kutimiza azma hiyo umakini na upembuzi yakinifu unatumika ili kuhakikisha mkopo wa benki unatumika kama ulivyokusudiwa, Mkopaji anapaswa kuhakikisha kwamba anazalisha pato ambalo linaloweza kulipa mkopo na kubakisha faida.
Si lengo la benki kuuza dhamana, mathalani mkopaji anaposhindwa kurejesha mkopo isipokuwa inabidi pale mkopaji anaposhindwa kutoa ushirikiana.

Maandalizi ya kukopa
Maandalizi ya kupata mkopo benki yanaweza kuchukua miaka zaidi ya mitatu kutokana na aina ya biashara. Kwanza kabisa tambua mahitaji ya msingi kabisa ya mkopo wa benki ni mawili. Moja ni biashara iliyoshamiri ikiwa na maana inayofanya vizuri kwa kutengeneza faida na mauzo mazuri ambayo yataonekana benki.
Pili ni dhamana kwa ajili ya uhakika kwamba fedha ya benki inarudi. Mahitaji haya mawili yatakusaidia ili utakapoingia benki unapewa kiti, soda au maji wakati ya ofisa wa benki akikusikiliza kwa makini kabisa.

Biashara inayofanya vizuri
Hakikisha biashara yako imesajiliwa na kupata vibali na leseni zote. Kukopa kunahitaji maandalizi, hakikisha fedha zote zinazopatikana kutokana na mauzo yako, unaweka benki na matumizi yako.

 Kama unahitaji kununua mzigo fedha itoke benki, lipia kodi za serikali kama inavyotakiwa, tunza kumbukumbu zako zote za biashara.

Pia kama unaweza kununua kompyuta, fanya hivyo ili ikurahisishie mahesabu yako katika kurekodi stoku na mauzo, fanya ukaguzi wa hesabu zako kwa wakaguzi waliothibitishwa na serikali.

 Usisubiri  kuambiwa na benki tunahitaji mahesabu yako yaliyokaguliwa, hapa unaweza kuingia gharama isiyo ya lazima na pengine usipate  mkopo. Pia hakikisha nyaraka zote zinatunzwa vizuri kwenye faili. Na mwisho ikatie bima biashara yako. 

Je, suala la dhamana linakuaje!!
Dhamana ziko za aina nyingi sana siyo tu nyumba na magari kama wengi walivyozoea, chamsingi lea biashara yako ili ivutie kukopesheka.

Suala la dhamana halitakuwa tatizo kwani hata ofisa wa benki ataweza kukushauri aina ya dhamana unayoweza kuweka kulingana na kiasi cha mkopo unaochukua. Dhamana ngumu nilizotaja  huchukuliwa kwa kuwa biashara nyingi zimekuwa na shaka na vihatarishi vingi.
Unapofanya biashara na kupata kipato kutoka vyanzo vingine jitahidi kuwekeza fedha zako kununua mali kama viwanja au nyumba ili baadaye ikusaidie kuwa dhamana, na pia unapopata kiwanja usikimbilie kujenga tu ovyo ovyo jipange jenga nyumba ya maana na yenye thamani ya kukupatia mkopo mzuri.

Pia jitahidi kujenga mahusiano na ndugu, jamaa na marafiki kadiri iwezekanavyo kwani wakiona biashara yako zaidi ya mwaka inafanya vizuri watakuwa tayari kukusaidia mali zao kudhamini mkopo wako benki.
Pia unaweza kuomba ushauri kutoka kwa watalaamu ili kujua aina ya dhamana za gharama nafuu unazoweza kuweka benki.
Mwisho, hakikisha unapokopa benki unakuwa mwaminifu kutumia fedha kama ulivyokusudia na kurudisha fedha hizo kwa wakati bila kukumbushwa wala kufikia hatua ya kuuza dhamana zako.
Benki ni rafiki wa mjasiriamali pale unapoonyesha ushirikiano mkubwa kwani tabia yako njema ya kukopa na kurudisha kwa wakati itakuwezesha kukopeshwa fedha nyingi zaidi hatimaye biashara yako itakuwa na kustawi zaidi

SIMBA SPORT CLUB YAICHAPA 4 - 0 SINGIDA UNITED.


Magoli ya Simba yalifungwa na Ramadhan,Ally,Omary na Singano.
.

0 comments:

Post a Comment