RAIS KIKWETE MKUTANONI BRASILIA, BRAZIL
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, Aprili 17, 2012 katika mkutano wa Open Government Partnership.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais wa Brazil Mama Dilma Rousseff alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, Aprili 17, 2012 kuhudhuria mkutano wa Open Government Partnership.
Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa Open Government Partnership ukibadilishana mawazo kabla ya ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, Aprili 17, 2012. Wa pili kutoka kushoto ni Waziri katika ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mh Mathias Chikawe, Waziri wa Kazi na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mh Haroun Ali Suleiman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Mahadhi J. Maalim na Msahuri wa Rais (Masuala ya Siasa) Dkt Laurian Ndumbaro.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa meza kuu na mwenyeji wake Rais wa Brazil Mama Dilma Rousseff na wajumbe wengine katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, Aprili 17, 2012 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Open Government Partnership. Kulia ni Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Bi Hilary Clinton.
Wajumbe wa Tanzania kutoka taasisi mbalimbali za kiraia na serikali wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, Aprili 17, 2012 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Open Government Partnership.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu wa Georgie Mh Nika Gilauri katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, Aprili 17, 2012 baada ya kuhudhuria mkutano wa Open Government Partnership.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mabalozi wa nchi mbalimbali wakati wa Mchapalo ulioandaliwa na Balozi wa Tanzania nchini Brazil Mh Francis Malambugi nyumbani kwa Balozi usiku wa Aprili 17, 2012 jijini Brasilia, Brazil.

PICHA NA IKULU

0 comments:

Post a Comment