Thursday, March 17, 2016



Rais John Magufuli na Mkewe, Mama Janeth leo amekuwa Rais wa kwanza Tanzania kupiga simu ya surprise moja kwa moja kwenye kituo cha runinga kama mtazamaji wa kawaida akichangia yaliyokuwa yanajadiliwa kwenye kipindi.

Magufuli amezungumza moja kwa moja na watangazaji wa kipindi cha ‘360’ cha Clouds TV akiwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya ikiwa ni pamoja na namna walivyochambua magazeti na mijdala mingine. Moja kati ya mijadala hiyo ilikuwa mjadala uliohusu ziara yake Benki Kuu.

Rais Magufuli pia aliisifu ‘Clouds Media Group’ kwa namna wanavyofanya kazi akiigusia tukio la ‘Malikia wa Nguvu’ lililolenga kutambua mchango wa wanawake nchini katika kuzitambua fursa na kuzifanyia kazi ipasavyo.

0 comments:

Post a Comment