Tuesday, September 10, 2013


Bila shaka umewahi kusikia ule wimbo wa njiwa peleka salamu! hahaha njiwa wanaaminika kutumiwa kupeleka ujumbe wa siri katika mambo mengi lakini mara hii ni ndege aina ya Mumbi (Swan) amekamatwa na kuwek
wa chini ya ulinzi huko Misri akidaiwa kuwa mpelelezi aliyetumwa na wafaransa.

Mapema wiki hii ndege Mumbi alikutwa nyuma ya jengo la gereza huko Qena akiwa amejikunyata huku mwilini mwake akiwa amefungwa kifaa cha elektroniki kilichodhaniwa kuwa ni cha upelelezi. Mkazi mmoja wa eneo hilo baada ya kumwona ndege huyo alimchukua na kumpeleka kwenye mamlaka ambako polisi walimuweka kizuizini (lupango).

Baada ya uchunguzi wa awali Mkuu wa mambo ya usalama wa Qena Ayman Abdallah alisema kifaa kilichofungwa kwa ndege huyo ni cha kufuatilia mwenendo na uhamaji wa ndege kinachotumiwa na wanasayansi wa Ufaransa na kuahidi kumwachia ndege huyo baada ya uchunguzi kumalizika.

Gazeti la serikali limempongeza mtu aliyehusika kumkamata ndege huyo kwa kuonyesha uzalendo wake na umakini katika kulinda maslahi ya taifa huku ndege huyo akiendelea kubaki korokoroni hadi hapo mamlaka zitakapokamilisha uchunguzi wote na kumwachilia huru.

Si mara ya kwanza kutokea matukio ya wanyama na ndege kudhaniwa kuwa ni wapelelezi hasa wakati wa vita na wakati mgumu kama wanaoupita Misri sasa.
Chanzo: NYDailyNews and abcLocal

0 comments:

Post a Comment