Monday, April 8, 2013

Dondooo:
  • Marais wa Tanzania, Kikwete na Dk Shein wamewaongoza wananchi katika dua ya kumwombea hayati  Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume aliyeuawa Zanzibar tarehe 7 Aprili 1972 huko Kisiwa Ndui yalipokuwa makao makuu ya ASP (Afro Shirazi Party) ambapo ndipo yalipo makao makuu ya CCM sasa.
Picture
Ofisi ambamo hayati Rais Abei Amani Karume aliuawa kwa kupigwa risasi (matundu yanaonekana ukutani)

  1. Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislam Tanzania imetoa wito kwa viongizo wa dini kuhakikisha hawawapi nafasi watu wasio na taaluma ya dini kuhusika kutolea ufafanuzi katika masuala ya kidini.
  2. Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amesihi Watanzania kuishi kwa kupendana na kuvumiliana hata katika kipindi hiki ambacho nchi inapitia changamoto nyingi.
  3. Majeruhi wawili waliobanwa katika ajali iliyolihusisha lori la mizigo katika eneo la Maseyu, Morogoro wameaga dunia baada ya kuchelewa kuokolewa kwa zaidi ya saa 16 licha ya wahudumu wa afya kujitahidi kutoa tiba katika eneo la ajali kwa muda wote. Wananchi wamedai marehemu hao wasingepoteza uhai endapo Serikali isingekosa vifaa, hali iliyolazimisha kuomba msaada kwa watu binafsi. 
  4. Baadhi ya wamiliki wa mabasi ya mikoani wamesema uamuzi wa Serikali wa kuongeza nauli za abiria, umezingatia kupanda kwa gharama za uendeshaji.
  5. Zaidi ya nusu ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kizigu katika manispaa ya Tabora, wanaketi chini kutokana na upungufu mkubwa wa madawati, hali ambayo inawapa adha kubwa wanafunzi pamoja na walimu.
  6. Wananchi wa Rwanda leo wamekumbuka mauaji ya kimbari yaliyotokeaa nchini humo mwaka 1994 na kusababisha kifo cha watu takribani milioni moja, ndani ya siku mia moja.
  7. Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba pamoja na Wabunge wawili wa CCM ambao pia ni wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM-NEC, wanaotoka katika jamii za kifugaji, Christopher Ole Sendeka na Lekule Laizer wamelazimika kufika Loliondo katika tarafa za Loliondo na Sale na kuzungumza na wananchi wanaoishi katika maeneo hayo katika jitihada za kuondoa tofauti zilizojitokeza hivi karibuni baada ya Waziri wa Mali Asili na Utalii kutoa kauli ya kumega eneo la pori tengefu la Loliondo kwa shughuli za uhifadhi. Ujumbe huo umeahidi kufikisha kero za Wananchi hao kwa Waziri Mkuu ili kupata ufumbuzi wake. Wananchi hao wamesema Serikali ifikirie na iache uamuzi wake wa kuwapa wawekezaji ardhi. Pia, wameitaka Serikali iwarejeshee ardhi hiyo ili iwapunguzie usumbufu na kuhangaika.
Taarifa saa 1 jioni - ZBC
Taarifa - TBC
Taarifa saa 2 usiku - Radio One Stereo

0 comments:

Post a Comment