Tuesday, April 16, 2013

Picture
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Luaha Kilosa Mkoani Morogoro wakati yeye akiongozana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wakati katibu mkuu huyo alipofanya ziara katika eneo hilo, Katibu mkuu huyo yuko katika ziara ya kikazi ya kuhimiza maendeleo na kukagua miradi ya maendeleo ili kuisimamia serikali katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwahamasiha wananchi katika kushiriki shughuli za maendeleo.
Katibu  Mkuu  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amewataka viongozi na wananchama wa chama hicho kubadilika na kuachana na tabia  ya kubeza kila hoja na malalamiko yanayotolewa na wapinzani  kwa niaba ya wanchi.

Katibu mkuu huyo ametoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara  uliofanyika kata ya Ruaha  wilayani Kilosa  ikiwa ni mkutano wake wa kwanza  mara baada ya kuanza ziara yake ya siku saba  mkoani Morogoro  kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi  na kukagua  utekelezaji wa ilani ya CCM.

Kinana amesema kuwa hoja zinazotolewa na wapinzani lazima zipimwe  na kufanyiwa kazi  badala ya kubezwa, akisisitiza kuwa tabia ya kubeza kila hoja ya wapinzani  imechangia viongozi wengi  kushindwa  kuwajibika kwa wananchi.

Baada ya kuwahutubiwa wananchi  katibu mkuu huyo akatoa nafasi kwa wananchi kuelezea kero zao na akalazimika kujibu baadhi ya hoja hizo ambapo kwa upande  wa kero za wakulima wa miwa amehadi kufikisha tatizo hilo kwenye kamati kuu ya CCM, CC .

Awali katibu mwenezi  wa CCM taifa Nape Moses Nauye  katika utangulizi wake amewapongeza wananchi  kwa ushiriki wao katika kutoa maoni ya katiba  na uundwaji wa mabaraza ya katiba

Praxeda Mtani, TBC Morogoro.

0 comments:

Post a Comment