Friday, December 7, 2012

Mwezeshaji wa mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa Habari juu ya Wajibu wa Vyombo vya Habari katika utekelezaji wa Soko la Pamoja la Jumuia ya Afrika ya Mashariki (EAC), Balozi Jeremy Ndayiziga, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo yaliyoliyoanza leo Jijini Dar es Salaam na kushirikisha waandishi kutoka nchi Wanachama wa EAC. Kulia ni Mtaalam wa Masuala ya Habari kutoka EAC, Sukhdev Chhatbar, ambaye pia ni mratibu wa mafunzo hayo. Balozi Ndayiziga ni Mtaalam katika Masuala ya Mtengamano wa EAC. 
Washiriki wakichangia mada katika mafunzo hayo ambayo yameandaliwa kwa pamoja kati ya EAC na Shirika la Kijerumani la GIZ. 
Washiriki wakifuatilia mada na michango ya washiriki wengine kwa umakini.
Mwandishi Mkongwe, Zephania Ubwani kutoka Mwananchi Communication Ltd, Arusha akichangia mada. Kulia ni Salma Said pia wa Mwananchi na DW Zanzibar.
Picha ya pamoja ya washiriki wote na wawezeshaji.
Mtaalam wa Masuala ya Habari kutoka EAC, Sukhdev Chhatbar, ambaye pia ni mratibu wa mafunzo hayo akijadili jambo na Mwanahabari Mkongwe na Mchambuzi wa Masuala ya Siasa za Afrika, Jenerali Ulimwengu. Ulimwengu pia ni Mwezeshaji katika Mafunzo hayo. 
Mkufunzi akiendelea na kutoa mada. Kulia ni Mkufunzi mwenzake Jenerali Ulimwengu akimsikiliza kwa makani na kushoto ni mshiriki mwandishi Kimeli arap Kemei kutoka Kenya.
Huu ulikuwa wakati wa Mtengamano kati ya Fiona na James 
Mercy na Fiona wakiwa mkutanoni
(picha, maelezo: Ayoub Mangi, Professional Photojournalist & BLOGGER, ayoubmangi.blogspot.)

0 comments:

Post a Comment