Friday, December 7, 2012

Picture: Shabani Matutu
Tanzania Daima na Sayari, Shaaban Matutu akionyesha jeraha lililotokana na kupigwa risasi na Polisi katika tukio lililotokea usiku wa kuamkia Jumanne – baada ya polisi kuvamia nyumbani kwake Tegeta jijini Dar es Salaam kwa madai ya kumtafuta mtuhumiwa waliyekuwa wakimsaka. Matutu kwa sasa amelazwa Hospitali ya Muhimbili katika Kitengo cha Mifupa (MOI) kwa ajili ya matibabu zaidi.(Picha: HakiNgowi blog).
Ndugu wapendwa,

DSM City Press Club imepata taarifa  za kushtusha kufuatia ya kupigwa risasi  na kujeruhiwa begani kwa mwandishi wa Tanzania Daima Bwana Shabani Matutu (30) ambaye pia ni mwanachama wa Dar City Press Club (DCPC).

Sambamba na taarifa hizo imeelezwa kuwa mwandishi huyo amelazwa katika Taasisi ya mifupa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI). Chanzo hasa cha kupigwa risasi kwa mwandishi huyo bado hakijaeleweka kwa DCPC, uongozi wa DCPC unafuatilia.

Tutakapojiridhisha na taarifa zilizotolewa pamoja na zile tutakazozipata tutawataarifu rasmi. Kwa sababu hizo tunaomba waandishi wote, ndugu, jamaa, marafiki, wapenda haki na amani, wanaharakati washirika na wadau wote wa vyombo vya habari kuwa watulivu tukimjulia hali kwa misaada ya hali na mali mwandishi mwenzetu Shabani Matutu ili apone majeraha.

Wenu katika ujenzi wa Taifa,
Joseph Kayinga
Katibu Mkuu

---
Soma zaidi taarifa za tukio hili kwenye gazeti la Mtanzania - Polisi wampiga risasi mwandishi wa habari - TanzaniaDaima - Jeshi la Polisi lajeruhi mwandishi kwa risasi na HabariLeo - Polisi wampiga risasi mwandishi wa Tanzania Daima.

0 comments:

Post a Comment