Tuesday, November 13, 2012

Picture
picha: militaryentrepreneur.org
Makala hii imeandikwa na Meshack Maganga-Iringa, Tanzania

Ndugu zangu,

Nimemaliza kusoma kitabu cha ‘Success Principles’ wiki hii,aidha, nimesoma makala ya mwandishi maarufu Freddy Macha kwenye gazeti la Mwananchi Jumapili tarehe 11 yenye kichwa ‘Maisha Bongo, Majuu hali moja’. Kwenye makala yake Freddy Macha ameeleza waziwazi kwamba wapo baadhi ya vijana wa kibongo ambao huota kwenda kuishi ‘majuu’ bila kujua kwamba huko maisha ni magumu kuliko hata bongo,na kwamba, popote pale unapoishi utawakuta watu wakilalamika na kusema kuwa afadhali kwenda mahali pengine. Kisha akaenda mbali kwakusema kuwa, ukijua na kutambua la kufanya na namna ya kumudu maisha,unaendelea na mapambano,kwa sababu kanuni kuu ya  uhai ni harakati.

Nakumbuka nilipokuwa kidato cha pili miaka michache iliyopita,baba yangu Mzee Maganga,alipata safari ya kwenda Uholanzi, kabla ya kuondoka aliniuliza ni kitu gani ambacho ningependa atakaporudi kutoka Uholanzi aniletee kama zawadi,nilimwambia aniletee vitabu vya kusoma, baadhi ya ndugu zangu walinicheka maana wao waliomba waletewe nguo.Baba aliporudi aliniletea kitabu maarufu cha Dr. Nomarn Vincent Peale, kiitwacho ‘THE POWER OF POSTIVE THINKING’,kiakili nikuwa mdogo ila kimenisaidia sana katika kujenga mtazamo sahihi wa maisha.

Ndugu zangu, kila siku binadamu anagundua mambo mapya ambayo yanamsaidia kumudu kupambana na mwendo na mabadiliko ya kasi katika maisha. Miongoni mwa ugunduzi mwingi wa hivi karibuni umekuwa ukihusu mawazo ya binadamu. Ugunduzi huu umesaidia kubadili mitazamo ya wanasayansi wengi, wakiwemo wale wa fizikia ambao kea muda mrefu wameonekana kukataa sana maelezo kwamba mawazo yana nguvu kuliko miili yatu.

Kila mmoja wetu ana namna yake ya kufikiri na hizi namna tofauti za kufikiri ndizo ambazo zinatutofautisha binadamu. Ni tofauti hizi pia ambazo zinatufanya tuwe na tofauti katika mafanikio maishani mwetu. Wale ambao wanafikiri vizuri na kuamini katika kumudu, huwa wanafanikiwa. Wale ambao wanafikiri vibaya na kiamini katika kushindwa, siku zote huwa wanaanguka.

Huenda ni vigumu kwa mtu kujua, huku kufikiri vizuri na kuamini katika kumudu ni kupi na pia huku kufikiri vibaya na kuamini katika kushindwa ni  kupi. Kwa bahati nzuri hayo yote yameelezwa kwenye mada nyingine zinazohusu kufikiri kitabuni humu. Kwa bahati nzuri zaidi, wataalamu wa masuala ya mawazo na mafanikio kama John Gray, Vincent Peale, Anthony Robbinins na wengine, wanabainisha vigezo ambavyo vinaweza kumfanya mtu kutabiri kama maisha yake yatakuwa ni ya kushindwa hadi mwisho au yatakuwa ni ya mafanikio.

Inailezwa kwamba, kama mtu akiwa anaamini kwamba kuna watu wengine wa aina Fulani mahali Fulani, ambao ndio peke yao wanaoweza kufanikiwa na kufika juu kwenye ngazi ya kimapato, mtu kama huyo hawezi kamwe maishani mwake kuja kutoka kwenye lindi la umaskini.

Hawezi kutoka kwenye lindi hilo kwa sababu juhudi zake ambazo zingemfikisha mbali zinakuwa tayari zimewekewa ipaka na imani hiyo, kwamba yeye hahusiki  katika kufanikiwa, bali kuna wengine ambao ni Mungu mwenyewe  anayewajua na aliyewateua. Kwa kufikiri hivo, juhudi yake kubwa  katika kutafuta itakuwa ni ile ya kumfanya asife tu kwa njaa na siyo kuvuka hapo. Kama ujuavyo, tunapoamini kuhusu jambo fulani, mawazo yetu hutusaidia kulifikia jambo hilo.

Kwa kuamini hivyo, mazingira tunayojenga ni yale ya kutusaidia kuishi kwa kupata riziki tu. Hata kama “fuko la fedha” litadondoshwa miguu mwetu tutalipiga teke na kuliambia “mimi sikuandikiwa kupata bwana, kuna wenyewe, hali kama hii hujitokeza mara nyingi sana maishani mwetu. Tunakabidhiwa dhamana kubwa ambayo ingetusaidia sana maishani mwetu, lakini tunacheza nayo hadi inapotea kwa sababu tu hatuamini kwamba utunastahili kuitumia kufika juu. Tunaziona nafasi za kusonga mbele, lakini tunaamini kwamba, hatustahili kuzitumia.

Fursa zikija waziwazi kabia, tunajifanya hatuzioni kwa kutafuta visingizio mbalimbali ili tusizitumie, kwa sababu tu, tumeamini kwenye mawazo yetu kwamba, sisi hatustahili. Ni vigumu kugundua kwamba nafasi au fursa hizo zimekuja kwa sababu tayari tumejifungia njia kuelekea mafanikio. Wengine kwa bahati baya wanaweza kuona na kubaki wameshangaa ni kwa nini tushindwa kuinuka katika mazingira tuliyomo.

Mtu ambaye anaamini kwamba hawezi, yaani ameshashindwa kutokana na sababu mbalimbali, anaelezwa na wataalamu wa elimu ya mafanikio kwamba, kamwe mtu huyu hawezi kuja kuvuka kizingiti cha umaskini. Kuna watu ambao kutokana na sababu mbalimbali walifanywa kuamini kwamba hakun wanchoweza. Wengine kutokanana malezi, mazingira au uzoefu mbalimbali wa kimaisha.

Mtu anapoamini kwama hawezi, anayaambia mawazo yake ya kina yamsaidie kumfanya ashindwe zaidi kwenye kila jaribio analofanya. Badala ya kufanya juhudi kujisaidia ili amudu, hujipweteka kwa kuamini kwake kwamba hata kama atafanya kitu gani, kamwe hatamudu. Siyo rahisi kwa mtu mwenye mawazo ya aina hii kuweza kufanikiwa maishani.
Kuna watu ambao kwa sababu ya kukosa kile ambacho jamii inakiona kuwa ndiyo ufunguo wa mafanikio, huwa wanaamini kwamba hawawezi kufanikiwa au kufanya vizuri maishani kama hao ambao wanacho. Kwa mfano, kwa kukosa elimu, ujuzi au utaalamu fulani, watu wengine hujihesabu kama wanyonge. Huchukulia kwamba ni wale tu wenye elimu, ujuzi na utaalamu fulani ndiyo wanaoweza au wanaotakiwa kufanikiwa.

Bila shaka umeshawahi kusikia au hata wewe mwenyewe kusema, “Si wamesoma bwana’ ndiyo wanaojaliwa, sisi ambao hatuna elimu kazi yetu itakuwa ni kuwatumikia. Kauli kama hizi zina chimbuko lake mbali sana, pengine katika malezi yetu. Wazazi kwalizoea au wamezoea kuwaambia watoto wao, “Usiposoma kazi yako itakuwa ni kuwabebea wenzako mizigo, unafikiri pesa inaokotwa, nk.  Kwa bahati mbaya mtoto aliyelishwa “sumu” (‘EARLY CHILD PROGRAMMING’) hii anaposhindwa shule, huamini kwamba yeye atabaki kuwatumikia wengine tu.

Tunapoamini kwamba kwa sababu hatuna elimu ya kutosha napengine ujuzi au utaalamu Fulani, hatuwezi kufika juu kwenye mafanikio, ni wazi hatutafika. Moja ya vigezo muhumu vinavyoweza  kutufikisha kwenye mafanikio ni kuamini kwetu kwamba tunaweza kufika huko. Tunapokuwa hatuna imani kwamba tunaweza kufika huko hujifungia njia wenyewe.

Baadhi yetu kuwa tunaamini kwamba tuna mikosi, balaa au nuksi napengine laana ambazo zinatuzuia katika kufikia malengo yetu. Tunaamini hivyo kiasi kwamba hata tukifikia karibu kabisa na mafanikio huwa tunajiambia ni kazi bure, tutaporomoka tu. Na kweli kwa kuamini hivyo hujikuta tukiporomoka kila tukifika karibu na kufanikwa au kufikia malengo.

Kinachotokea ni kwamba, kwa kuamini kwetu kuwa tunamkosi, balaa, laana au nuksi, huwa tunatenda kwa mkabala huo wa kinuksi au kibalaa na kimkosi, ambapo matokeo yake ni kujikwamisha. Watalaamu wa elimu ya mafanikio wanaeleza kwamba tunapoamini kuwa tuna mkosi au nuksi huwa tunayashauri mawazo yetu ya kina kutusaidia kuendelea kuwa katika hali hizo (Niliwahi kufafanua zana hii nilipoandika makala ya BINADAMU NI ZAIDI YA MWILI WAKE). Ndiyo maana siyo rahisi  kukuta mtu anayeamini katika nuksi akiondoka katika hali hiyo.

Tufanyeje basi, kama ni kweli kimapato tuko hoi napengine tunachoweza ni kupata riziki yetu ya kila siku tu? Pamoja na kwamba mengi yameelezwa  tayari kwenye mada nyingine, bado tunaweza kukuambia, tunachotakiwa kufanya ni kujenga imani ya kumudu. Kamwe hatutakiwi kabisa kujiambia tulipofikia ndipo basi, hatuwezi kupanda zaidi.

Hebu soma kwa makini habari hii: Mwaka 1997, Pablo alikuwa  ni mtu wa kuishi kwa kubahatisha. Alikuwa akifanya vibarua hapa na pale na maisha yalikuwa magumu sana kwa upande wake. Hakuwa na matumaini kabisa kwamba ingetokea siku akasimama. Siku moja akiwa kwenye kibarua chake, alimsikia mtoto wa tajiri yake akisema, “Baba haiwezekani, tusikate tamaa ni Lazima tutaweza, kwani wanaoweza wana mkataba gani na Mungu?, ni lini waliongea na Mungu na kuhakikishiwa kwamba wangekuja kupata?. Tujipe moyo wa kuweza halafu tufanye…” ITAENDELEA.

0 comments:

Post a Comment