Friday, January 18, 2013

Muuguzi mwandamizi Gladness  Msemo, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka manne likiwamo la kughushi cheti cha muuguzi mwandamizi.

Katika shitaka la kwanza, Wakili wa Serikali, Keneth Sekwao, alidai kuwa mshitakiwa anadaiwa kuwa katika tarehe na mahali pasipojulikana jijini Dar es Salaam, alighushi cheti Na.13421 akijidai kuwa kilitolewa na Baraza la Wauguzi Juni 20, mwaka 1995.

Katika shitaka la pili, mshitakiwa alidaiwa kuwa Februari, mwaka 2006 alitoa hati ya uongo ya cheti cha uuguzi chenye Na. 13421 kwa Gustav P. Moyo.

Katika shitaka la tatu, mshitakiwa anadaiwa kuwa tarehe, mwaka na mahali pasipojulikana, alighushi cheti chenye Na. 13421.

Kuhusu shitaka la nne, ilidaiwa kuwa Julai 10, mwaka 1987, mshitakiwa alitoa hati isiyokuwa ya kweli yenye Na. 10199 akidai kuwa imetolewa na Baraza la Wauguzi.

---
via gazeti la NIPASHE

0 comments:

Post a Comment