Tuesday, November 6, 2012

Picture
photo: catholicweb.com
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Mhashamu Tarsicius Ngalalekumtwa, anasikitika kutangaza kifo cha Mhashamu Askofu Aloysius Balina  wa Jimbo Katoliki Shinyanga, kilichotokea leo mchana wa tarehe 06 Mwezi 11 Mwaka 2012 katika Hospitali ya Rufaa Bugando kwa saratani (cancer) ya ini.

Mipango ya Mazishi inafanywa.

Habari ziwafikie Maaskofu wote wa Kanisa Katoliki Tanzania, Mapadri, watawa, waamini wote, ndugu, jamaa, marafiki na wote wenye , mapenzi mema popote pale walipo.

Marehemu Askofu Aloysius Balina alizaliwa katika kijiji cha Isoso Bariadi katika Mkoa wa Shimiyu tarehe 21 Juni 1945, alipata Daraja Takatifu la Upadri tarehe 27 Juni 1971 na akateuliwa na Baba  Mtakatifu John Paul II kuwa Askofu wa Kwanza wa Jimbo Katoliki  la Geita tarehe 8 Novemba 1984.

Aliwekwa Wakfu kuwa Askofu wa Geita tarehe 6 Januari 1985 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro huko Roma.

Tarehe 8 Mwezi Agosto 1997 aliteuliwa na Baba Mtakatifu John Paul II kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga na akasimikwa Jimboni Shinyanga tarehe 17 Novemba 1997.

Amefariki dunia tarehe 06 Novemba 2012 akiwa na umri wa miaka 41 hivi ya Upadri na 27 ya Uaskofu.

Aloysius Balina (amezaliwa 21 Juni, 1945) ni askofu Mkatoliki nchini Tanzania. Aliwekwa wakfu na Papa Yohane Paulo II mwaka wa 1984. Tangu 1997, ni askofu wa Jimbo la Shinyanga.

0 comments:

Post a Comment