Tuesday, November 6, 2012

 
 
 
 
 
 
 

Baadaye wandesha pikipiki, “boda boda” walivamia kituo cha mafuta wakitaka kuthibitishiwa kuwa hakuna mafuta.
KITUO CHA ORXY 
 Vijana wa boda boda wakiwa wamevamia kitu cha mafuta cha ORXY wakitaka kujua kama kweli hakuna mafuta.
 Hapa kila mtu anataka kushuhudia kama mafuta yapo au hayapo
 Meneja wa kituo hicho aliyevaa shati jeupe akijaribu kuwatuliza wateja ambao wana jazba kubwa ya kutaka kujua ikiwa kuna mafuta ama la, na kuwaambia wangoje achukue vifaa ili awaoneshe hali halisi.
 Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mbeya naye alikuwepo katika eneo la tukio ili kuwatuliza vijana hao na kuwahakikishia kuwa wataoneshwa ukweli. 
 Hapa katikati wanapotazama ndipo penye tanki la mafuta na vijana hao wanasubiri kushuhudia. 
 Hapa kazi ndiyo inaanza ya kuhakikisha kuwepo au kutokuwepo kwa mafuta kwa kutumia chuma maalumu ambacho huingizwa katika matanki hayo 
 Vijana wanahakikisha na kuthibitishiwa kuwa ni kweli, hakuna mafuta ya petroli katika kituo hicho cha ORXY
Picha na Ayoub Mangi

0 comments:

Post a Comment