Tuesday, November 6, 2012

Picture
Mohamedi Mtoi
Picha zinawaonesha wanafunzi waliokuwa katika chumba cha darasa wakifanya mtihani wa Taifa wa kidato cha pili ulioanza jana nchini kote Tanzania.

Wanafunzi hawa walianza kusinzia mmoja mmoja ilipogonga nusu saa tu baada ya muda wa kuanza mtihani wa Hisabati ambao ulipangiwa saa mbili. Wanafunzi walionekana hoi huku wengi wakizikusanya karatasi zao za mitihani bila kuandika majibu ya maswali zaidi ya matatu.

wavuti.com inayo video inayoonesha wanafunzi karibu wote wakiwa wamesinzia, ila kwa sababu za kimaadili, video hiyo haitawekwa hapa ili kuwasitiri baadhi ya wanafunzi ambao sura zao zinaonekana dhahiri.

Ikiwa unataka maelezo ya ziada, tafadhali wasiliana na MohamediMtoi

0 comments:

Post a Comment