Tuesday, October 30, 2012

Habari imeandikwa na Nathaniel Limu via DewjiBlog

Mtoto mmoja mwenye umri wa miezi minne amepoteza maisha baada ya kukeketwa, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake tarehe 28/10/2012, kamanda wa polisi mkoa wa Singida, Linus Sizumwa, alimtaja mtoto huyo wa kike aliyefariki dunia baada ya kukeketwa, kuwa ni Shamila Saidi.

Alisema tukio hilo la kinyama na la kusikitisha, limetokea oktoba 27 mwaka huu saa kumi alfajiri, huko katika kijiji cha Mwanyonyi tarafa ya Ilongero jimbo la Singida kaskazini.

Alisema kuwa siku ya tukio, mama mzazi wa mwathirika huyo Tausi Kassimu (24) alimpeleka mtoto wake kukeketwa na garaiba Amina Nkungu, ili aweze kupona ugonjwa wa kuharisha na kutapika. Magonjwa  hayo yanadhaniwa  kusababishwa na ugonjwa wa lawalawa.

Sizumwa alisema baada ya kukeketwa,mtoto huyo alivuja damu nyingi na kupelekea kifo chake.

“Hadi sasa tunamshikilia mama yake na mtoto huyo, ambaye ni Tausi Kassimu na watu wengine Sakina Swalehe (24)  na Asha Salum (60) wote wakazi wa kijiji cha Mwanyonye. Ngariba Amina Nkungu alifanikiwa kutoroka lakini tumeanzisha msako mkali, ili tumkamate aweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria”, alisema kamanda huyo.

0 comments:

Post a Comment