Tuesday, September 25, 2012

Jumla ya warembo 30 wanataraji kuingia kambi ya REDDS MISS TANZANIA 2012 wakati wowote baada ya kumalizika kwa mashindano ya Vitongoji, Mikoa, na hatimaye Kanda mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa mashindano hayo ya Kanda ambayo kila Kanda imetoa washindi wa tatu ambao wataziwakilisha Kanda zaoi katika Shindano hilo kubwa na laiana yake.Warembo hao na Kanda zao wanazotoka ni Redds Miss Kanda ya Kaskazini Warida Frenk, Anande Raziel na Lucy Stefano, Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012 ni  Rose Lucas, Irine Veda na Joyce Baluhi , Redds Miss Kinondoni Brigit Alfred, Diana George Hussein na Irene David.

Kanda nyingine ni Redds Miss Lake zone 2012 Eugene Fabian,Happiness Daniel na Happiness Rweyemamu, Redd's Miss Tameke 2012, Edda Sylvester, Flavian Maeda na Catherine Masumbigana, Redds Miss Kanda ya Kati, Belinda Mbogo, Lightness Michael na Elizabeth Diamond.Washiriki wengine watakao ingia Kambini ni kutoka kanda ya Redds Miss Ilala 2012, Mary Chizi, Magdalena Munisi na Noela Michael, Redds Kanda Vyuo vya Elimu ya Juu, Virginia Mokiri, Fatma Ramadhani na Fina Revocatus, kanda nyingine ni ya Kutoka Chuo Kikuu Huria ni Zuwena Nassibu na Redds Miss Southern Zone Naomi Jones, Caren Elias na Venance Edward.Kesho Septemba 26, 2012 Kamati ya Miss Tanzaniaikiongozwa na Mkurugenzi wake Hashim Lundenga kutoka Lino International Agency watakutana na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maeleo majira ya saa 4:00 asubuhi kuzungumzia maandalizi ya Kambi hiyo.
Redds Miss Lake zone 2012/13 Eugene Fabian (katikati) akiwa pamoja na , mshindi wa Tatu Happiness Rweyemamu na Kulia kwake ni mshindi wa pili Happiness Daniel warembo hawa wataingia kambi ya REDDS Miss Tanzania 2012.
------------------------------------------------------------- 
Redds Miss kanda ya Kaskazini Warida Frenk katikati akiwa na washindi wenzake Anande Raziel kulia na lucy stefano kushoto mara baada ya kutawazwa kuwa washindi wa Redds Miss Kanda ya kaskazini,Washindi hao wanatarajiwa kujiunga kwenye kambi ya Redds Miss Tanzania hapo baadae ili kujiandaa na shindano la Taifa la Redds Miss Tanzania.
Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas katikati akipunga mkono kwa furaha akiwa na mashindi wa pili Irine Veda (kulia) na Mshindi wa tatu Joyce Baluhi mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo lililofanyika mjini Morogoro usiku wa Septemba Septemba 1, mwaka huu. Warembo hawa wote watashiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2012 baadae mwaka huu.
Mshindi wa shindano la Redds Miss Kinondoni Brigit Alfred, akiwapungia mkono mashabiki walioshuhudia shindano hilo jijini Dar es Salaam jana, kulia ni mshindi wa pili Diana George Hussein na mshindi watatu Irene David. Brigit pia anashikilia taji la Redds Miss Sinza 2012 huku Irine akishikilia taji la Miss Ubungo 2012.
Malkia wa Redd's Miss Tameke 2012, Edda Sylvester (katikati), akiwa na mshindi wa pili Flavian Maeda (kushoto), pamoja na Catherine Masumbigana aliyeshika nafasi ya tatu katika kilele cha mashindano hayo, Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
 Naomi Jones, Caren Elias na Venance Edward
Redds Miss Kanda ya Kati, Belinda Mbogo (katikati) akiwa na mshindi wa pili Lightness Michael (kushoto) na mrembo aliyetwaa nafasi ya tatu Elizabeth Diamond baada ya kumalizika kwa shindano hilo mjini Dodoma hivi karibuni. warembo hawa wote wameingia kambi ya Miss Tanzania 2012.
Redds Miss Ilala 2012, Noela Michael akiwa na mshindi wa pili Magdalena Munisi (kulia) na mshindi wa tatu Mary Chizi (kushoto) mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Redd's Miss Ilala 2012.

0 comments:

Post a Comment