Friday, September 28, 2012


MSANII mahiri anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu bongo Rose Ndauka, asema kuwa baada ya kuwa kambini kwa muda mrefu akitengeneza kazi ambazo awali alizitaja sasa zimekamilika na Octoba zinaenda sokoni ambazo ni ‘Upofu’ na ‘Special Cover’ huku zote zikiwa zimefanyika chini ya kampuni yake inayojulikana kama Ndauka Entertainment.
Awali msanii huyo alisema kuwa filamu hizo zipo kwenye mchakato wa kupigwa picha lakini sasa ameamua kuweka wazi kuwa kila kitu kimekamilika na mwezi ujao zitakuwa sokoni kwa ajili ya kuwapa uhondo mashabiki.Ndauka alisema kuwa ameamua kutoa filamu mbili kwa mpigo kwani mashabiki wake wana hamu ya kuona kazi nyingi zaidi na nzuri kutoka kwenye kampuni yake pia malengo yake ni kujitangaza zaidi kimataifa.

“Nakumbuka niliwahi kusema Octoba nitakuja na filamu mbili kutoka kwenye kampuni yangu kazi zipo tayari hivyo kinachosuburiwa ni ratiba ifike ili mashabiki wangu waweze kuona utamu wa kazi zangu, ujio huo utakuwa ni mzuri kwani utaifanya Kampuni yangu iweze kujulikana zaidi kimataifa” alisema.

0 comments:

Post a Comment