Sunday, September 9, 2012

Na Khatimu Naheka
MSHAMBULIAJI hatari wa Timu ya Yanga aliye kwenye chati kwa sasa, Said Bahanuzi amefanyiwa kitu mbaya katika mtandao wa kijamii maarufu kama Facebook.
Mwanandinga huyo alipatwa na masahibu hayo kufuatia mtu asiyejulikana kufungua akaunti kwa kutumia jina la straika huyo hatari na kuanza kuwasiliana na watu mbalimbali ambapo wengi walikuwa wakiamini wanawasiliana na Bahanuzi.
Akichezesha taya na Udaku Spoti, Bahanuzi alisema hajawahi kujihusisha na masuala ya Facebook na kusema hajui lolote juu ya mtandao huo lakini amemlaani vikali mtu huyo anajifanya ni Bahanuzi kwani anamchafulia.
“Kusema kweli sijui lolote juu ya Facebook na sijawahi kufungua kwa kuwa haijawahi kunivutia, sasa nashangaa huyo aliyefungua kwa kutumia jina langu, kibaya zaidi amechukua picha zangu na kuanza kuwasiliana na watu na wengi wamekuwa wakiwasiliana naye wakidhani ni mimi wakati siyo,” alisema Bahanuzi.

0 comments:

Post a Comment