Sunday, September 2, 2012

Picture
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa, Mwandishi wa Habari, Daudi Mwangosi (pichani) wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten amefariki dunia katika ghasia zilizozuka kati ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na polisi katika mkutano wa chama hicho mkoani Iringa jioni hii.

Pia askari polisi mmoja wa Wilaya ya Igowole anasemekana yuko mahututi kutokana na kipigo. Taarifa kamili kuhusiana na tukio hili zitawajia baadaye. --  Kutoka kwenye blogu ya Ziro na Tina
                                                                    

Picture

Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel TEN cha Iringa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Iringa, (IPC) AMEUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI, WAKATI POLISI WALIPOFYATUA MABOMU WAKATI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikiwa katika Tawi katika Kijiji cha Nyororo, wilayani Mufindi, mkoani Iringa. -- Kutoka kwenye blogu ya Mkwinda                                                                                   
                                           _______________


Daud Mwangosi ameuwawa leo katika vurugu za Polisi na wafuasi wa CHADEMA katika kijiji cha Nyololo, Mufindi, Iringa.

Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za CHADEMA Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi.

Kabla ya kuuawa kwa mwanahabari huyo, mabomu yalipigwa eneo hilo ili kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa, Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadaye mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini.

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti.

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa CHADEMA kurushiana mawe kwa mabomu, zaidi ya magari matano ya CHADEMA na ya wananchi yameharibiwa, huku watu kadhaa wakiachwa wamejeruhiwa hali mwanahabari mmoja, Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya. --- Kutoka kwenye blogu ya FrancisGodwin, Iringa. (pamoja na picha zinazoonekana hapo chini, bofya picha moja moja kusoma malezo yaliyopo chini yake)

0 comments:

Post a Comment