Thursday, May 10, 2012



Agness Gerald ‘Masogange’ .

 Aunty Ezekiel Grayson.
Na Mwandishi Wetu
SKENDO nzito imewaibukia mastaa wa Bongo, Aunty Ezekiel Grayson na Agness Gerald ‘Masogange’ wakituhumiwa kumtapeli fedha mbunge maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Kwa mujibu wa mbunge mwenyewe (jina limehifadhiwa), alianza mawasiliano kwa kutumia mtandao wa kijamii wa Facebook na mrembo aliyeandika jina lake Aunty Ezekiel.
Akasema mawasiliano yalinoga, ikafika mahali ‘Aunty’ huyo akatoa shida yake kwa mheshimiwa ambapo alimtaka wakutane amsaidie kiasi cha fedha ili kutatulia tatizo lake.
“Ukaribu wetu kupitia Facebook ulinoga sana nikijua ni Aunty Ezekiel, akanipa na namba yake. Kuna siku akanitumia ujumbe (SMS) kwamba ana shida, anaomba fedha, nikamwelekeza tukutane mahali f’lani nimpe.
“Lakini wakaja wasichana wawili, yeye akaniambia ameshindwa kutoka ana tatizo, niliwapa fedha wale aliowatuma,” alisema mbunge huyo.
Aliendelea kuweka wazi kuwa mawasiliano kati yake na ‘Aunty’ huyo yaliendelea na alizidi kumsaidia kwa hali na mali katika matatizo yake.
Kwa mujibu wa mbunge huyo ambaye pia ana cheo kikubwa bungeni, siku moja alikutana na Aunty ‘laivu’ na kumtaiti kwamba ni kwa nini anashindwa kukutana naye uso kwa uso wakati ameshamsaidia sana.
“Cha kushangaza, Aunty alikataa kuwasiliana na mimi na akasema hajawahi kujiunga na Facebook hata siku moja.
“Nilishtuka, lakini pia nilishangaa sana. Kumbe kuna warembo hapa mjini wanaishi kwa njia haramu kiasi hiki?” alimalizia mbunge huyo.
Amani lilimsaka Aunty kwa njia ya simu na alipopatikana na kusomewa mashitaka yake alikiri kukutana na mheshimiwa huyo na kumpa malalamiko hayo.
“Ni kweli nilikutana na huyo ….(akamtaja jina), akanisimulia hayo unayoniambia, nikakataa kuwasiliana na yeye, akasema hata namba yangu eti anayo.
“Nilimuomba namba hizo, nilipoziandika kwenye simu yangu likatokea jina la Masogange (Agness). Hii ilinishangaza sana. Lakini ukweli ni kwamba mimi sihusiki jamani,” alisema kwa masikitiko makubwa staa huyo.
Amani lilimpandia hewani Masogange na kumpa ‘ei tu zedi’ ya mheshimiwa, naye akafunguka:
“Mimi sijawahi jamani, pengine kuna mtu anatumia jina langu kujinufaisha kwa watu wakubwa, lakini siyo mimi. Na hii inaweza kunichafulia sana.”
Alipoulizwa kama alishawahi kulalamikiwa na Aunty juu ya matumizi ya jina lake, mrembo huyo alisema:
“Yes! Aliwahi kuniambia, nikamjibu kama nilivyokujibu wewe kwamba sihusiki kabisa.”

0 comments:

Post a Comment