Thursday, May 10, 2012

.
Baada ya shilingi milioni tisa kupelea katika milioni 25 zilizohitajika kumpeleka mwigizaji Sajuki kwenda India kutibiwa, Mwigizaji Jackline Walper yeye mwenyewe amejitolea dola za kimarekani elfu kumi zaidi ya milioni 15 za kitanzania kwa ajili ya matibabu ya Sajuki.
Mtangazaji Shadee wa Clouds TV ameripoti kwamba “shukrani kubwa ya Sajuki aliyoitoa ni kutokana na kiwango hicho kikubwa cha pesa ambacho kimemaliza kabisa hitaji la pesa nyingine zilizokua zimepelea ambapo mbali na hayo kampuni ya Dallas Entertainment inamsimamia msanii huyo kwa malazi na chakula kwa kipindi chote atakachokuepo India”
Hata hivyo Mwenyekiti wa Bongo Movies Club JB amesema kuna ulazima pia kwa wao kama bongo movies kuchangishana ili kuweza kumpa Jackline Walper pesa alizozitoa ambapo mpaka sasa kiasi cha pesa kilichokusanywa kwa ujumla ni dola elfu ishirini.

CHANZO CHA HABARI  http://millardayo.com

0 comments:

Post a Comment