Monday, May 7, 2012

Ubao wa matokeo katika uwanja wa taifa ulivyosomeka
Klabu ya soka ya Simba, imesherehekea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara msimu huu kwa staili ya aina yake baada ya kushusha mauaji ya kukumbukwa kwa mahasimu wao wakuu Yanga pia ya jijini Dar es salaam.
Katika pambano la kumaliza ligi hiyo lililowakutanisha miamba hao jioni ya leo kwenye uwanja mkubwa wa taifa jijini Dar es salaam, Simba waliingia uwanjani wakiwa na nia ya kujenga heshima kwa kukabidhiwa ubingwa wakiwa wamemfunga mtani wao huku Yanga ambayo imekuwa kwenye mgogoro wa ndani kwa ndani hivi sasa, ikiwa na nia ya kuhakikisha wanapunguza machungu ya kupokonywa ubingwa kwa kumuangusha mnyama.
Hata hivyo, ni Simba, ambao walifanikiwa katika lengo lao baada ya kuwashindilia vijana hao wa Jangwani jumla ya mabao 5-0 huku mabao matatu kati ya hayo yakiwekwa kimiani kwa njia ya matuta kutokana na beki za Yanga kuwafanyia rafu wachezaji wa Simba.
Bonyeza hapa na hapa kuona kilichowaathiri Yanga hadi kupoteza ubingwa, kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa na kukumbana na gharika la Msimbaazi leo hii.

0 comments:

Post a Comment