Simba
imebeba wachezaji wake wote kwenda mjini Tanga kuwavaa Coastal Union
katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Jumamosi. Lakini imewaacha
wachezaji hawa wanne.
Kwanza
ni Hija Ugando na Mohammed Fakhi ambao ni majeruhi, Hassan Isihaka
aliyesimamishwa na Hassan Kessy mwenye kadi tatu za njano.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano cha Simba, Haji Manara amethibitisha hilo.
Simba
ndiyo vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 54 wakifuatiwa
na Yanga na Azam FC, kila mmoja akiwa na pointi 50, wanapishana idadi ya
mabao ya kufunga na kufungwa.
0 comments:
Post a Comment