Friday, July 12, 2013


fikra ni mbegu ya kile unachotarajinayo hutoa sawia na kilichopandwa
                                   
Nimeamua kuandika makala hii kujadili jambo muhimu sana,na endapo utachukua nafasi kujifunza na kusoma mara kwa mara utatambua mambo mengi
Mwisho wa makala hii utatambua mambo yafuatayo
        I.           (a)  Wewe ni mjenzi na mbomoaji wa maisha yako
      II.           (b)  Mazingira yanayokuzunguka ni matokeo ya fikra zitokazo ndani mwako
    III.            (c) Jinsi gani unaweza kubadili maisha yako.
    IV.             (d)  Dunia mpya.
Mara nyingi tunapomuona mtu akifanikiwa katika biashara tunasema ana bahati’ama kismati’.Tunapomuona mwenzetu akifanya vizuri katika elimu tunasema Mungu amembariki na kumpa akili nyingi,TUKIONA WENGINE WAKIFANYA UGUNDUZI tunasema ‘ana akili nyingi’.Hatutakumbuki jambo moja,ya kuwa kuna magumu wanayoyapitia watu hawa mpaka kufikia mafanikio lakini kubwa zaidi ni kwamba kabla ya matokeo hayo,walianza kufikiri,kisha wakaweka nia ili kutimiza malengo hayo ambayo sasa yanaonekana wazi.
Ukiona simu,kumbuka kuwa aliyetengeneza alianza na fikra juu ya mawasilano,akafanya juhudi mpaka kufika hapo.Ukiitazama TELEVISHENI,Kumbuka kuwa haikugunduliwa kwa bahati mbaya bali ilianza na mtu kufikiri.Ukiona kuna uoto mzuri nyumbani kwa mtu,si kwamba ulitokea kwa bahati mbaya,ulianza na wazo ndani ya muhusika,kisha akafanya juhudi kutekeleza.
Kila unachokiona ,unachokitumia ni matokeo ya fikra za watu na wewe ukiwa mmoja wao.Marimba,Kinanda,kijiko,sahani,gari,baiskeli na vingine vingi vijavyo ni matokeo ya fikra za wanadamu.
Hakuna jambo hata moja ama ugunduzi wowote uliojitokeza katika mazingira rahisi,fikra ilianza kufanya kazi,ikasukuma hamu ya kufikia ndoto hizo,na mwisho wa siku..jambo lililokusudiwa linatimia
Kujenga maisha yako kunaanza na fikra zako.Unapata kadiri unavyofikiri.Unapoweka fikra juu ya jambo,unapata matokeo yake kadiri unavyofikiri.
Huwezi kutenganisha kile kilichopo ndani ya fikra za mtu na kile akitendacho ama ambacho kinaonekana.Kinachoonekana ,ni matokeo ya fikra za mtendaji.Vivyo hivyo huwezi kutenganisha kati ya ulimwengu wa kiroho na  ulimwengu unaoonekana kwa macho..Uonekanao kwa macho ni matokeo ya ule wa kiroho (usioonekama kwa macho).Katika elimu ya Saikolojia unaweza kupima  fikra na tabia kwa kutazama matokeo ya mambo yanayotendwa na mtu .
Mazingira bora ya kuishi hayatokei kwa bahati mbaya,yanajengwa na fikra (mtazamo).Mtazamo chanya huyajenga,nao mtazamo hasi huyabomoa.Hivyo ni wazi kuwa unapotaka kupata mafanikio katika jambo lolote,unaanza na fikra chanya juu ya jambo hilo,Jifunza kutazama kila jambo katika mtazamo chanya. Kila mmoja wetu ana ndoto ( matarajio ) ya kufnya jambo Fulani maishani,na kuwa mtu Fulani maishani…Unachokiwaza ndicho kitakachotokea katika uhalisia.Fikra ni mbegu ya kuelekea mafanikio.Ukipanda mbegu ya fikra chanya,utavuna kama ulivyopanda,vivyo hivyo ukipanda hasi,utavuna ulivyopanda.Ukiona vyaelea ,vimeundwa.
                                  UNAWEZA KUBADILI MAISHA YAKO
ni wewe ndio uliye msanifu wa maisha yako
                                
                                        
Kwa maelezo hayo ,unaweza kubadili maisha yako kwa kubadili fikra zako.Unaweza ukawa katika mazingira magumu sana,lakn kamwe hutabaki hivyo kama utaanza kuwaza vyema,fikra za mafanikio,upendo,amani zinakupelekea kwenye matokeo chanya
Mawazo uwazayo juu yako ni kipimo unachojipimia katika mwenendo na matokeo ya maisha yako.Matokeo yake kamwe hayajifichi.Hatuchagui mojakwa moja juu ya mtiririko wa maisha yetu,lakini kupitia fikra,tunachagua matokeo ya maisha yetu na kuujenga mtiririko wa maisha yetu.
Fikra huonekana matokeo yake haraka kwenye tabia,na tabia huleta matokeo ya maumivu ama furaha (majuto ama furaha).Kwa kifupi tabia uliyonayo,iletayo matokeo yake ya majuto ama furaha ndiyo inayotoa picha ya fikra iliyotoa msukumo wa matokeo hayo..
Fikra yenye woga,wasiwasi,na kutowajibika huonesha tabia ya unyonge , kutojiamini na kutochukua hatua,matokeoa yake ni kukata tamaa, kushindwa na kuwa tegemezi kwa kila jambo.
Nazo fikra  yenye uvivu hupelekea tabia za udhaifu/unyonge, udanganyifu(usanii sanii) na matokeo yake ni kuwa ombaomba,masikini na uzembe.(ukiona nchi ina kila rasilimali,na inakuwa masikini,basi ujue watu wake wote ni wavivu kufikiri na wasipobadili fikra hizo watabaki kuwa ombaomba hata kama matrilioni ya pesa yatatolewa kama msaada)
Fikra za chuki na kutojiamini huleta tabia za visasi na uonevu,matokeo yake ni vurugu,kutoweka kwa amani,mauaji ya kutumia nguvu.Unaweza kujifunza matokeo ya viongozi wasiojiamini na wenye chuki.
Fikra za ubinafsi (umimi) huleta tabia ya ushindani,unyang’anyi,(roho mbaya tunaita waswahili).Na matokeo yake kila mmoja anayajua.
Kwa upande mwingine fikra zote njema  huleta matokeo mema kwa watu wote.
Fikra za kutia moyo,kujiamini na kuchukua hatua huonekana katika tabia za utu wema na kuwajibika,matokeo yake ni amani,mafanikio na uhuru wa kweli.
Huwezi kuwa huru mpaka utakapokuwa na fikra huru.Ukifahamu jinsi unavyoweza kubadili maisha yako kwa kubadili fikra zako…umeyafikia mafanikio
Mkononi mwako ni matokeo halisi ya kile ukiwazacho….maisha yako unayoyaishi sasa ni matokeo halisi ya fikra zako,kwa kutambua ama kutotambua.Unavuna ulichopanda.Hakizidishwi wala kupunguzwa.Ukiachilia mbali hali uliyonayo sasa,unao uwezo wa kubadili maisha yako…ama kubaki ulivyo.Hii ni kwa kupitia mawazo yako mwenyewe. Utarudi nyuma kama mawazo yako yanavyotaka,ama utasonga mbele kama mawazo yako yanavyotaka.Mawazo hutoa msukumo moyoni.Msukumo huo huleta matokeo sawia.
Kama utasubiri mazingira ya mafanikio yako yajengwe na mtu mwingine(wengine) basi utasubiri mpaka mwisho..Ni wewe na wala si mwingine wa kuchukua hatua.Juhudi  huleta matokeo.Kiwango cha juhudi unayoiweka,kinatanabaisha juu ya matokeo yake. Fikra unazozijaza katika mawazo yako,msukumo unaouweka moyoni mwako ndio ujengao maisha yako,na ndivyo utakavyokuwa.
                                                    DUNIA MPYA
                Dunia mpya ni matokeo ya fikra zako mpya.Dunia mpya ni ile inayojengwa na wale wanaoamini katika uwezo walionao.Dunia tunayoishi sasa,mazingira yake,hali yake ni matokeo ya fikra zetu wanadamu.Kuongezeka kwa joto,kutoweka kwa amani na upendo,uchoyo,wivu ni matokeo ya binadamu yaliyoanza muda mrefu.Dunia mpya yenye amani,furaha,upendo,usawa,hali bora inajengw na sisi ,kila mmoja akichukua hatua juu ya fikra zake na maamuzi yake.Mimi binafsi naiona dunia mpya,yenye amani na furaha,upendo na maelewano,dunia hii itajengwa na watu wenye fikra za usawa,upendo,umoja baada ya dunia inayojengwa na wenye chuki na matabaka kushindwa.Love never fail

0 comments:

Post a Comment