Wednesday, March 27, 2013

Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Jakaya Mrisho Kikwete amefunga rasmi mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ya muda mfupi kwa viongozi. Mafunzo hayo yalidumu kwa muda wa majuma matatu na kufungwa rasmi jana, Machi 25, 2013.

Zifuatazo ni baadhi ya picha kutoka kambi mbalimbali. 
Picture
Wakiwa shambani pamoja ni Wabunge Zitto Kabwe, Iddi Azzan, Abdallah Haji, Raya Ibrahim na Antony Mbassa kwenye kambi ya Mgambo 835KJ.
Picture
Zitto Kabwe akijiandaa kwenda katika gwaride la mwisho
Picture
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anayefuata ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azzan, wakiwa kwenye Paredi ya kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT Kikosi cha 835 Mgambo JKT kambi iliyopo katika Kata ya Mgambo ilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Picture
Mbunge wa Kinondoni Iddi Azzan pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ZItto Kabwe, wakihitimu mafunzo ya JKT katika kambi ya 835 Mgambo JKT iliyopo Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Picture
Mbunge wa Kinondoni Iddi Azzan, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Picture
Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT huko Kibaha Mkoani Pwani.
Picture
Wakiapa mbele ya kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga.
Picture
Mbunge Viti maalum Raya Khamis , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni.
Picture
Mbunge wa Kiwani Pemba, Abdallah Haji Ali, , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Picture
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi kutoka kwa kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Picture
Mbunge wa Biharamulo, Dk Athanas Mbassa, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. picha na Hussein Semdoe.
Picture
Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dk Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi, mbunge wa viti maalum Ester Bulaya leo katika kambi ya Ruvu JKT.
Picture
Baadhi ya waliokuwa katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
(picha zote via Mtaa kwa Mtaa blog)

0 comments:

Post a Comment