Wednesday, March 27, 2013

Imeandikwa na Happiness Katabazi via blog

ANAYEDAIWA kumuua askari wa kikosi cha Usalama Barabarani wiki iliyopita, Elikiza Nnko, Jackson Stephen Fimbo jana alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na makosa ya matatu likiwemo kosa la kuingilia msafara wa kiongozi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Kwey Lusema wakili mwandamizi wa serikali Lasdilaus Komanya alilitaja kosa la kwanza  ni la kusababisha  kifo cha trafiki huyo  kupitia kwendesha gari kwa hatari  na kwamba Machi 18 mwaka huu,  katika barabara ya Bagamoyo katika mataa ya Bamaga jijini Dar es Salaam,  mshitakiwa akiwa ni dereva  kiongozi wa gari lenye namba za usajili  T328 BML aina ya Land Rover Discovery.

Wakili Komanya alidai mshitakiwa huyo  aliendesha gari hilo ka mwendo wa hatari  katika barabara hiyo ambayo ni ya umma, jambo ambalo  linahatarisha  usalama wa raia. Kutokana na mshitakiwa huyo kuendesha gari hilo kwa mwendo huo wa hatari, alimgonga askari huyo ambaye amezikwa Alhamisi iliyopita.

Alidai kosa la pili ni  kuingilia msafara  wa kiongozi, kwamba siku ya Machi 18 mwaka huu, katika eneo hilo la mataa ya Bamaga, mshitakiwa huyo hakutii  maelekezo yaliyokuwa yakitolewa kwa ishara ya askari Elikiza, ambaye alikuwa na wajibu wa kuyasimamisha magari kwa njia ya ishara.

Wakili Komanya alidai shitaka la tatu ni la kushindwa kutoa  taarifa za kusababisha ajali katika barabara hiyo ya umma katika kituo chochote cha jirani.

Mshitakiwa huyo alikanusha mashitaka hayo.

Wakili Komanya alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarahe ya kuja kumsomea maelezo ya awali mshitakiwa.

Kwa upande wake  hakimu Lusema alisema ili apate dhamana ni lazima awe na wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini bondi ya Shilingi milioni mbili, Mshitakiwa huyo alitimiza masharti hayo ya dhamana na akapata dhamana na hakimu huyo akaiarisha kesi hiyo  Aprili 15 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya upande wa Jamhuri kumsomea maelezo ya awali.

Katika hatua hutua nyinge, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi ya kuchapisha makala ya uchochezi inayomkabili aliyekuwa Mharii Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima na wenzake, kwa sababu Kibanda bado amelazwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini kwaajili ya matibabu na hivyo ameiarisha hadi Aprili 29 mwaka huu.

Picture
Akiongea jambo na wakili wake (mwenye koti jeusi) mara baada ya kesi kuahirishwa.

0 comments:

Post a Comment