Sunday, February 3, 2013

.
Picha ya jengo la PPF ikionesha moshi mkubwa unaofuka kutoka kenye jengo hilo (Shukurani ya picha: A, rafiki wa M.C.)

Taarifa zafahamisha kuwa, huenda hitilafu ya umeme iliyotokea kwenye mitambo ya mawasiliano iliyopo katika chumba cha 11, kilichopo  juu, mwisho kabisa mwa jengo la minara ya PPF lililopo kwenye makutano ya Ohio/Garden Avenue, katikati ya jiji la Dar es Salaam ndiyo iliyosababisha moto asubuhi ya leo majira ya saa moja u nusu hivi, na kusababisha jengo hilo ushika moto.

Imetaarifiwa kuwa walinzi  wa  jengo hilo  walishuhudia moshi mzito  ukitoka ndani ya  jengo hilo la ghorofa, ndipo walipotoa taarifa kwa vikosi vya zima-moto.

Kikosi cha uokozi kilifika kwa wakati katika eneo husika na pamoja na kuweko nyenzo katika jengo hilo za kukwea hadi orofa ya kumi na moja, ufupi wa mipira ya zima-moto ili kufikisha maji kwenye chumba kinachowaka moto ulikwamisha jitihada za kuuzima moto huo. Hata na hivyo, juhudi zilizofanywa na kikosi hicho zimefanikiwa kuuzima moto huo kuzima kabisa mnamo mwendo wa saa tano kasoro za adhuhuri.

Polisi wapo katika eneo hilo ili kulinda mali zisiporwe au kuharibiwa na vibaka.

Hakuna madhara yoyote ya moja kwa moja kwa binadamu yaliyoripotiwa. Thamani ya hasara iliyosababishwa na moto huo nayo haijafahamika.
.

0 comments:

Post a Comment