Wednesday, January 30, 2013

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, TMA, inauhadharisha umma kuhusu hatari ya uwezekano wa kuwepo kwa mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo nchini kutokana na kimbunga “FELLENG”.

Baadhi  ya maeneo ya mikoa  ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara  na maeneo jirani ya mikoa hiyo huenda yakapatwa na mvua kubwa  (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kila siku) kati ya tarehe 30  Januari, 2013 hadi 01 Februari, 2013.

Kimbunga “FELLENG” cha Kaskazini-Mashariki mwa Madagascar kinavuta upepo wenye unyevunyevu kutoka Congo kupitia maeneo tajwa. Mamlaka inaendelea kufuatilia hali hiyo.

Tafadhali tizama picha ya satelite na kusoma taarifa kamili ya hali inavyoonekana wakati taarifa hii ikitolewa.

0 comments:

Post a Comment