Tuesday, January 29, 2013

KAMERA za blogu ya Dustan Shekidele asubuhi ya Januari 15, 2013 ilimemnasa mwanaume huyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja akivuka barabara eneo la Lunna katikati ya mji wa Morogoro huku akiwa amebeba mtoto mgongoni na kichwani akiwa na  godoro ambalo alitoka kulinunua kwenye moja ya maduka yaliopo eneo hilo.

Kuna baadhi ya wanaume wanafikira potofu kwamba jukumu la kulea watoto linawahusu wanawake pekee jambo ambalo sio la kweli, jamaa huyu amedhihirisha kwa vitendo jambo hilo kwa kutembea na mtoto wake mgongoni katikakati ya mji wa Morogoro bila kuwa na wasi wasi wowote na maneno au macho ya watu.

picha, maelezo: Dustan Shekidele, Morogoro.

0 comments:

Post a Comment