Friday, January 18, 2013

Madiwani wawili wanaoziwakilisha kata mbili ndani ya Manispaa ya Bukoba wamechapana makonde baada ya kutokea mabishano katika kikao cha maadili chenye lengo la kumshinikiza Mh. Meya, Anathory Amani  ajiuzuru.

Madiwani  hao waliotwangana kuzua tafrani kubwa hadi kufikishwa kituo cha polisi ni Diwani wa Kata ya Kahororo, Mh. Chief Kalumuna na Diwani wa Kata ya Nyanga Mh. Deusdedit Mtakyawa wote wanachama wa Chama Cha Mapinduzi - CCM.

---
via Bukoba Wadau blog

0 comments:

Post a Comment