Tuesday, January 29, 2013

Picture
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya siasa na viongozi wa Asasi mbalimbali kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA mjini Mtwara Januari 27, 2013
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda yupo Mkoani Mtwara akikutana na makundi ya wadau mbalimbali wa mkoa huo ili kusikia kutoka kwao mawazo, michango na dukuduku zao kuhusu mradi wa gesi asilia.

Imeripotiwa kuwa Waziri Mkuu angekutana na wanahabari baadaye leo saa 9 alasiri ili kutoa mjumuisho wa maongezi yake. Taarifa mpya zitawekwa hapa punde zitakazopatikana. Kwa sasa, tafadhali sikiliza rekodi ya kipindi cha Amka na PRIDE FM radio, kilichozungumzia muhtasari wa yaliyojiri katika kikao cha jana kati ya Waziri Mkuu na Wadau.

(Pleya zipo za aina mbili ili kuongeza wigo wa uchaguzi wa urahisi wa kifaa chako kwa ajili ya kusikiliza.)
Mtwara na Waziri Mkuu - PRIDE FM


UPDATES/TAARIFA MPYA za ziara ya Waziri Mkuu kutoka kwa Baraka Mfunguo - MtwaraKumekucha blog

Waziri Mkuu alikuwa akutane na Waandishi leo saa tisa alasiri. Kutokana na kikao kirefu cha madiwani wa Manispaa ya Mtwara/Mikindani na Mtwara vijijini pamoja na kikao cha wafanyabiashara, majumuisho ya ziara ya Mtwara atayatolea ufafanuzi kesho.

Kwa sasa (jioni) anakula chakula na kikao cha Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mtwara kitafuatia.

Kutokana na kuwepo kwa makundi katika Kamati ya Siasa ya CCM-Mkoa, wabashiri wengi wanasema kikao hicho kitakuwa na mvutano mkali.

Dondoo muhimu:

  • Kwa ufupi wajumbe wengi wamekataa bomba la gesi lisiende Dar
  • Wamemkataa Mkuu wa Mkoa na kumtaka Waziri Mkuu aondoke naye
  • Wajumbe (Madiwani ) kumpinga kwa kauli moja  Hawa Ghasia kwa kile kilichosemwa kutumia mamlaka  kutoa kauli za uongo kuhusu Mtwara Vijijini kuunga mkono suala la gesi iende Dar madiwani waMtwara vijijini. Wamesema hawakushirikishwa.
  • Mzozo wa viwanja baina ya Madiwani na Mkuu wa Wilaya
  • Waziri Mkuu ametumia mbinu ya kisiasa kuwashawishi Wadau kuwa bomba liende Dar
  • Wajumbe wameondoka kwa shingo upande kwa kukubali kutokubaliana na Waziri Mkuu
  • Kikao kinafanyika chini ya ulinzi Mkali wa FFU, JWTZ na UwT (Usalama wa Taifa)
  • Hawa Ghasia arudishwa Uwanja wa Ndege, JKNIA asije Mtwara kwani anaweza kuchafua hali ya hewa
  • Polisi wanadai Meya anataka kuwachonganisha na jamii/wananchi kutokana na kauli yake ya kusema wao ndio chanzo cha vurugu

0 comments:

Post a Comment