Tuesday, January 29, 2013

Lulu) akizungumza na wakili wake Peter Kibatala muda mfupi kabla ya kuanza kusikilizwa ombi lake la dhamana leo asubuhi (picha: Raha za Pwani blog)
Taarifa ya habari ya saa saba machana kupitia TBC imesema:
Msanii wa filamu Elizabeth Michel, maaruf kama Lulu, anayekabiliwa na shitaka la tuhuma za mauaji ya aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba, leo amepewa dhamana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam.

Masharti ya dhamana hiyo ni pamoja na:

- Kuwa na wadhamini wawili kwa dhamana ya Shilingi milioni 20 kila mmoja
- Kukabidhi pasi yake ya kusafiria kwa Msajili wa Mahakama
- Kuripoti Mahakamani kila tarehe Mosi ya kila mwezi.
- Marufuku kusafiri nje ya nchi.
Taarifa kwa kina kama ilivyowandikwa na Happiness Katabazi Happiness Katabazi

HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imempatia masharti matano ya kupata dhamana kwa msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael ‘Lulu’, anayekabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.

Masharti hayo yaliyolewa jana na Jaji Zainabu Mruke muda mfupi baada ya mawakili wa Lulu, Peter Kibatara, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe kuiomba mahakama hiyo impatie dhamana mshtakiwa huyo ambaye anasota rumande tangu April mwaka jana ambapo walieleza kuwa ombi la dhamana wameliwasilisha chini ya kifungu cha 148(1) ,(2) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 .

Jaji Mruke alisema ili mahakama impatie dhamana ni lazima asalimishe  kwa Msajili wa mahakama hiyo hati ya kusafiria,  kutotoka nje ya Dar es Salaam  bila ruhusa ya mahakama, kuripoti kwa msajili kila mwezi, kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali  ambao watasaini bondi ya Sh. milioni 20 kila mmoja.

Baada ya jaji huyo kutangaza masharti hayo Lulu na wakili wake walitoka nje ya ukumbi uliokuwa ukiendeshwa kwa shauri hilo kwa ajili ya kwenda kwa msajili kutimiza masharti hayo lakini kwa bahati mbaya Msajili hakuwepo ofisini na hivyo kufanya Lulu kurudishwa rumande hadi leo atakapoletwa kwa ajili ya kujatimiza masharti hayo mbele ya Msajili wa mahakama hiyo.

Kufuatia mahakama hiyo kumpatia masharti ya dhamana Lulu kutoka na ombi lake Na.125/2012 la kuomba mahakama hiyo impatie dhamana, bado kesi ya msingi inayomkabili Lulu ambayo ni ya kuua bila kukusudia haijapangiwa jaji wala tarehe ya kuanza kusikilizwa.

Desemba 21 mwaka jana, Hakimu Mkazi Christine Mbando wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu aliifunga kesi ya kuua bila kukusudia Lulu na kuiamishia rasmi kesi hiyo katika Mahakama Kuu, na uamuzi huo wa mahakama ulitokana na upande wa Jamhuri kumsomea maelezo ya kesi yake kwa kina mshtakiwa huyo na kuieleza mahakama kuwa wanakusudia kuleta jumla ya masha
hidi tisa.

0 comments:

Post a Comment