Monday, December 31, 2012

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki (CHADEMA), Joshua Nassari, amedai kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdluhaman Kinana ni hatari kwa rasilimali za taifa.

Akizungumza kwenye mkutano wa upatanisho kwa viongozi wa chama hicho, uliofanyika viwaja vya mpira Karatu Nassari aliishangaa CCM kwa uamuzi wake wa kumteua Kinana.

“Kinana amepewa dhamana kukisafisha CCM wakati yeye mwenyewe ni mchafu. Amechaguliwa wiki moja tu rasilimali zetu zikakamatwa huko China, huku Kampuni yake ikihusishwa kwa karibu. Kule Meru tumempiga marufuku kwasababu tuna hifadhi ya Taifa pale ya Arusha, sasa nanyinyi huku Karatu kwasababu mpo karibu na Hifadhi ya Taiga, angalieni sana hawo Tembo wenu,” alisema Nassari.


---
via gazeti la MTANZANIA

0 comments:

Post a Comment