Sunday, November 11, 2012








Questions

Mwambu, Salome Daudi  [CCM]
Iramba Mashariki Constituency
Session No Question No To the Ministry of Sector Date Asked
8 174 REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT Local Government 11 July 2012
Principal Question No
Walimu hucheleweshwa sana kupandishwa
madaraja na pia pale wanapohamishwa hawalipwi
posho za uhamisho ambazo wanatakiwa walipwe na hivyo kuwavunja moyo na kusababisha matizo ya migomo na kadhalika:-

(a) Je, Serikali itamaliza lini matatizo ya walimu ili nao waishi kama wafanyakazi wengine wa Serikali?

(b) Je, Serikali itachukua hatua gani kwa
Wakurugenzi Watendaji wanaochelewa kuwasilisha “Seniority list” ambayo hutumika kupandishia vyeo watumishi?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #174 SESSION # 8
Answer From Hon. Majaliwa, Kassim Majaliwa
REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT
NAIBU WAZIRI, alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri
Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Salome
Daudi Mwambu, Mbunge wa Iramba Mashariki, lenye
vipengele (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua
umuhimu wa walimu na kuthamini mchango wao
mkubwa katika kutoa elimu nchini. Kwa kutambua
hilo, Serikali imekuwa ikiboresha huduma kwa
watumishi wote nchini wakiwemo walimu na kuchukua
hatua mbalimbali kumaliza matatizo ya walimu
ikiwemo; kuboresha viwango vya mishahara, posho
nyingine ambazo watumishi au mtumishi anastahili kwa mujibu wa Kanuni.

Sheria na Taratibu zilizopo, kutenga fedha za
malipo ya stahili mbalimbali ikiwemo uhamisho katika Bajeti za kila mwaka na kutoa maelekezo kwa
Wakurugenzi wote wa Halmashauri kuhakikisha
kwamba uhamisho unafanyika pale tu ambapo fedha
zimetengwa kwa ajili hiyo.

Katika mwaka wa fedha 2011/2012, Serikali ilitenga
jumla ya shilingi bilioni 15.8 kwa ajili ya uhamisho kwa walimu wa Shule za Msingi na Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ilipata jumla ya shilingi milioni 131.5.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakurugenzi
Watendaji kwa mujibu wa ratiba kila robo mwaka
wanatakiwa kuwasilisha orodha ya ukubwa kazini
(Seniority list) kwenye Mamlaka za Wizara na Tume ya Utumishi. Halmashauri zimeendelea kuandaa na
kuhuisha kwa wakati orodha ya ukubwa kazini ili kuwa na taarifa sahihi za watumishi. Aidha, Serikali inaendelea kuwasisitiza Wakurugenzi kutekeleza
majukumu yao ipasavyo na kuhakikisha kwamba
taarifa zinazohitajika zinaendelea kuwasilishwa katika Mamlaka husika kwa wakati husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni Serikali
kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (ORMUU), imeanzisha matumizi ya mfumo shirikishi wa taarifa za kiutumishi na mishahara (Human Capital Management System) ambao utapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ucheleweshaji wa taarifa za watumishi kuhusiana na upandishwaji wa madaraja.

0 comments:

Post a Comment