Wednesday, November 14, 2012

Rais Jakaya Kikwete amechaguliwa kuwa Mwenyekiti  wa CCM kwa kura  2395 kati ya 2937 zilizopigwa  ambazo ni sawa na asilimia 99.92%

Akitangaza matokeo hayo Spika wa Bunge la Tanzania ambaye ndiye alikuwa msimamizi, Anne Makinda alisema kwamba Mwenyekiti  alipata ushindi wa kura 2,395 kati ya kura 2,937 zilizopigwa, kura mbili zilisema hapana.

Makamu Mwenyekiti Zanzibar Dkt. Ali Shein alipata kura 2,397 wakati makamu kwa upande wa Bara ndugu Phillip Mangula naye alipita kwa asilimia mia moja.

Wajumbe 20 wa viti vya Bara na Zanzibar ni kama ifuatavyo:

Nafasi kumi za NEC Zanzibar:

  1. Mbarawa Mnyaa - 1,850
  2. Mohammed Seif Khatib - 1,668
  3. Khadija Hassan Aboud - 1,625
  4. Shamsi Vuai Nahodha - 1,603
  5. Dkt. Hussein Mwinyi - 1,579
  6. Samia Suluhu Hassan - 1,525
  7. Omar Yussuf - 1,485
  8. Bhawanji Misuria Mshamba - 1,406
  9. Abdulhakim Cosmas Chasamma - 1,248
  10. Khamis Mbeto - 1,233

Nafasi kumi za NEC Tanzania Bara:

  1. Wassira Stephen - 2,135
  2. January Makamba - 2,093
  3. Mwigulu Nchemba – 2,012
  4. Shigella Martine - 1,824
  5. Lukuvi William - 1,805
  6. Membe Bernard - 1,455
  7. Mathayo David - 1,414
  8. Mukama Wilson - 1,374
  9. Msome Jackson - 1,207
  10. Mukangara Fenella – 984

0 comments:

Post a Comment