Friday, November 2, 2012

Timu ya MoBlog imezunzumgumza na Mama Mzazi wa mwanamuziki Rehema Chalamila al maaruf Ray C na hii ni taarifa yake:

Mwanamuziki wa kike Rehema Chalamila maarufu kama Ray C kwasasa anaishi maisha magumu baada ya kuathiriwa na kinachosemekana  kuwa ni matumizi ya madawa ya kulevya kwa muda mrefu.

Mwanadada huyo maarufu kama kiuno bila mfupa hivi karibuni alihamishia makazi yake mjini Nairobi , Kenya, na aliporejea nchini hali yake ilikuwa mbaya.

Akizungumza na Mo blog kwa njia ya simu, mama mzazi wa Ray C,  Bi Margret Mtweve amesikitishwa na kitendo cha vyombo vya habari kuandika tu hali ya Ray C bila kuhamasisha msaada.

“Kwa kweli mwanagu ninaye nyumbani kwa sasa nalala naye kabisa, na nimeokoka namuombea sana kwa Mungu, na ninaamini Mungu ni mwema atamsaidia” alisema Bi Margret nakuongeza:  “Mwanangu aliwasaidia watu wengi lakini sasa hivi ana matatizo sioni mtu hata mmoja wa kuja kunipa msaada, zaidi ni simu za waandishi kutaka habari za kumchafua”

Mama Ray C yuko tayari kupokea msaada wowote kutoka kwa wanajamii na namba yake ya simu ni 0655 999 700 waweza mtumia hata kwa Tigo Pesa.

Picture
Nakala ya gazeti via MillardAyo.com

0 comments:

Post a Comment