Wednesday, November 14, 2012

WAKATI Chama cha mapinduzi kikikamilisha mchakatowake wa chaguzi zilizo anzia tangu ngazi ya shina na kufikia kilele chake ngazi ya taifa leo huko Kizota mjini Dodoma kuna mambo mengi tumejifunza.

Pamoja na mambo mengine mengi yaliyojitokeza kwenye chaguzi hizo yakiwemo madai ya kukithiri kwa rushwa ambazo hata Mwenyekiti wa Chama hicho kushitushwa na rushwa hiyo lakini raha za pwani inaangazia uchaguzi wa viongozi wa kuu pekee wa chama hicho, maana kwa msimamo wa blog hii ndio uliotia kichefuchefu kuliko chaguzi za ngazi zote.

KUNAJISI DEMOKRASIA.

Kwenye hili sitaki kutafuna maneno nisemewazi kabisa CCM kinapaswa kuacha milango ya demokrasia iwe wazi kwa kilamwenye nia ya kugombea nafasi yeyote ndani ya chama bila kuingiza neno la utamaduni wetu tunaachiana. Kitendo cha kuwaweka wagombea watatu wote wanapigiwa kura za ndio na hapana kana kwamba hakuna wana ccm wengine ni kuinajisi demokrasia. Hata kama ni utamaduni basi unazorotesha demokrasia na kuondoa kabisa ladha ya uchaguzi, swali hapa linakuja itakuaje siku ikitokea rais mwenye hulka za kipekee akawa anafanya apendavyo bila kufuata matakwa ya chama huo utamaduni mtauondoa? Siitakua unyanyasaji kwani wengine wote wamefanyiwa hivyo?

MFUMO WA UPIIGAJI KURA.

Ilikuweka demokrasia wazi na ishike mkondowake na watu wapige kura bila ya kuogopa kushughulikiwa CCM ilipaswa iweke vituo vya kupigia kura hata vitano mle ukumbini halafu watu wapige kura badala ya utaratibu uliotumika wa kuwatoa kafara makatibu wa mikoa kusimamia mikoa yao kwenye upigaji wa kura. Yani hapa kila mkoa unapiga kura kwenye sandukulake halafu mwishowasiku mkoa uliopiga kura ya hapana unajulikana na hatimae hata watu waliopiga wataonyeshwa vidole sasa hapa demokrasia ikowapi?

MATOKEO YA KURA ZA VIONGOZI WAKUU.

Kwenye matokeo hapa ndio panazidi kutia kichefuchefu ati kwenye watu 2397 waliopiga kuraa tunaambiwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar Dk. Shein amepata kura zote na Makamo Mwenyekiti bara Philip Mangula amepata kura zote na JK ndio amekataliwa kwa kura mbili. Kwenye akili ya kawaida watu 2397 wanaopiga kura kwenye chama ambacho hadi wanakwenda kwenye uchaguzi kulikua na makundi ya kutaka madaraka ya viongozi hao wenye majukumu mengi yapunguzwe. Lakini hata katika hali ya kawaida haiwezekani wasiwepo watu wanaowapinga kutogombea watu hao, ila suala la vitisho na ubabe ndio viliwafanya wapiga kura wawe kama wamepumbazwa na kubadilisha misimamo yao. Kwa misingi hiyo Chama cha mapinduzi kwakua pamoja na kujivua gamba haitoshi kinapaswa kitumie mkorogo ili kiondoe mabaka mwilini maana bado kinajichafua ngoziyake. "


WAKATABAHU


Ayoub Mangi 

0 comments:

Post a Comment