Wednesday, October 31, 2012


 
Picture
Mwili wa Mwanafunzi wa darasa la tatu, Shule ya Msingi Iwambi, Jijini Mbeya Kervin Patrick (8) jinsia ya kiume ukiwa umefunikwa baada ya kufariki dunia kutokana na kujinyonga kwa kutumia kamba ya viatu katika bomba ya maji nje ya nyumba yao. (Picha: Ezekiel Kamanga, Mbeya)
MbeyaYetu blog: WANAFUNZI WA DARASA LA TATU AJINYONGA KWA KUTUMIA KAMBA YA VIATU

Picha, Habari kutoka kwa Ezekiel Kamanga, Mbeya.

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Iwambi, darasa la tatu Kervin Patrick (8) jinsi ya kiume amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya viatu katika bomba ya maji nje ya nyumba yao.

Tukio hilo limetokea Oktoba 27 mwaka huu majira ya saa 5 kamili usiku wakati wazazi wote wa mtoto huyo Bwna Patrick Mwakapalila (52) na Bi Subira Patrick (30) wakiwa hawapo nyumbani na kwamba baba mzazi akiwa na mwanae wa kiume aitwaye Joshua Patrick (10) waliondoka majira ya saa 3:30 kuelekea mjini.

Aidha Baba wa mtoto huyo alipigiwa simu na mtu mmoja kwamba arejee nyumbani na yeye pasipo kuchelewa alirejea na kumkuta mwanae amejinyonga katika bomba la maji kwa kutumia kamba ya viatu na chini kukiwa na ndoo, ambapo kifo hicho kimezua maswali mengi kwani kimo cha mtoto ni zaidi ya futi mbili na nusu na urefu wa kamba hali inayotia shaka kuwa mtoto huyo alichukua uamuzi huo yeye mwenyewe.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Ivwanga Bwana Chonde Kalisto amethibitisha tukio hilo la kusikitisha na kwamba yeye alipokea taarifa kutoka kwa Balozi wake Bi Esther Mahenge ambapo walitoa taarifa polisi ambapo walifika eneo la tukio kisha kuuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi na hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.
Picture
Mama mzazi wa marehemu Kervin Patrick (8)Bi Subira Patrick(38) akiwa katika hali ya majonzi kufuatika kifo cha mwanae aliyejinyonga. (Picha: Ezekiel Kamanga, Mbeya)
Picture
Baadhi ya majirani waliojitokeza kushuhudia mwili Mwili wa Mwanafunzi wa darasa la tatu, Shule ya Msingi Iwambi, Jijini Mbeya Kervin Patrick (8), (Picha: Ezekiel Kamanga, Mbeya)
SongeaHabri blog: APIGWA MSHALE NA KUFA PAPO HAPO -SERENGETI 
MWANAFUNZI WA SEKONDARI ATUHUMIWA KUUA KWA MSHALE

Imeandikwa na Anthony Mayunga-Serengeti.

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika sekondari ya Busawe kata ya Majimoto wilayani Serengeti mkoani Mara Peter Lucas Wambura(17)anasakwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga mshare kifuani Chacha Damiani Mangali(18) na kufa papo hapo.

Tukio hilo linalodaiwa kutokea oktoba 26, majira ya saa 2 mwaka huu usiku nyumbani kwa marehemu Mangali limethibitishwa na uongozi wa kitongoji na polisi linahusishwa na wivu wa kimapenzi.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho Daud Mgendi aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni jilani yake na marehemu alimpiga mshare kifuani na kufa papo hapo wakati anafungua mlango atoke nje ya nyumba yake.

“Sababu hazijajulikana kuwa ni vijana waliokuwa wanalingana huenda wamegongana kwa wanawake, maana inaonekana marehemu alifungua mlango akidhani ni mambo ya kawaida ndipo akapigwa mshare kifuani na kupiga kelele kisha akakata roho”alisema Mwenyekiti.

Alisema mara baada ya kutenda unyama huo mtuhumiwa aligeuka kama kichaa na kitishia usalama wa wananchi kwa kuwa alikuwa na upinde na mishare mingi ,na kutokana na giza walishindwa kumdhibiti na kutokomea kusiko julikana.

“Kumdhibiti ilikuwa vigumu kwa kuwa alionekana kuwa kama kichaa na kutishia watu kwa kurusha mishare ovyo na kutokana na giza kila mtu aliamua kuchukua tahadhari kwa kuwa hakuwa katika hali ya kawaida”alisema.

Baba mzazi wa marehemu Damiani Mangali akiongea na gazeti hili kwa njia ya simu alisema kuwa kijana wake alikuwa hajaoa na wanahisi huenda wamegongana kwa wanawake kwa kuwa hakuna madai mengine ambayo ameyasikia.

“Kama ingekuwa deni tungesikia lakini kwa matatizo ya wanawake mara nyingi huwa siri zao maana wote walikuwa vijana na majilani, nilipigiwa simu na kaka yake na marehemu kuhusiana na tukio hilo, tunaendelea kufuatilia chanzo lakini inauma kifo cha ghafla namna hii bila hata kuwaeleza sababu”alisema.

Polisi wilayani hapa waanaendelea na uchunguzi ikiwa ni pamoja na kumsaka mtuhumiwa ,ambapo wameomba wananchi watoe ushirikiano wa chanzo na alikojificha kwa kuwa anaweza kusababisha madhara makubwa zaidi.

Hivi karibuni mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili Mugumu sekondari wilayani wilayani hapa Mwang’omba Kegocha(16)amefikishwa katika mahakama ya wilaya kwa tuhuma ya kumchoma kisu Chacha Pasta (29)

Tukio ambalo linadaiwa lilitokea wakati wanacheza kamali ambapo mtuhumiwa inadaiwa alikuwa ana mdai marehemu ths 5,000 na katikakudaiana wakakorishana ndipo akamchoma kisu ubavuni na kufa papo hapo.
Picture
Baadhi ya mashuhuda wakiwa wamekusanyika kushuhudia Mwili wa Mkazi wa Kitongoji cha Gezaulole, Kijiji cha Haporoto Kata ya Ihango Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya Mbwiga Mwandele(50 -55) amejinyonga kwa kutumia mkanda wa Suruali yake katika Ofisi ya kijiji hicho. (Picha: Ezekiel Kamanga, Mbeya)
Picture
Mke wa marehemu Mbwiga Bi Malita Mbwiga (45) wa pili kutoka kulia akiwa na baadhi ya akina mama waliofika kumfariji kufuatia kifo cha mumewe (Picha: Ezekiel Kamanga, Mbeya)
Gazeti la HabariLeo: VISU VYAKATIZA UHAI KWA WIVU WA MAPENZI

WAKATI mvuvi kutoka Kambi ya wavuvi ya Kakoma – Kilangawana katika Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, Evod Luvanga (32), akidaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma kisu akimtuhumu kumdhalilisha, mwanamke mmoja jijini Dar es Salaam, amemchoma kisu na kumuua mchumba wake kwa sababu za kimapenzi.

Luvanga anadaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma kisu ubavuni akimtuhumu kumdhalilisha mbele ya rafiki zake kwa kumdhihaki kuwa mkewe ni ‘mzinifu aliyekubuhu’.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alithibitisha mauaji hayo yalitokea juzi katika kambi hiyo ya wavuvi usiku wa manane, ambako mtuhumiwa anadaiwa kumuua kwa kumchoma kisu ubavuni mkewe aitwaye Ales Mwanja (20) na kumsababishia umauti.

Kwa mujibu wa baadhi ya wavuvi kutoka kambi hiyo, walidai mtuhumiwa wivu dhidi ya mkewe ulikuwa ukiwaka kwa nguvu ndani yake, kwani alidai anampenda sana na hatakuwa tayari katika maisha yake kusikia ana mahusiano ya kimapenzi na mwanamume mwingine zaidi yake.

Inadaiwa kuwa kutokana na tabia yake hiyo ya kujigamba kumpenda sana mkewe, wenzake walianza kudhihaki iweje ampende kiasi hicho mkewe wakati ni ‘mzinifu’, hali iliyomkwaza mtuhumiwa ambaye aliahidi kuifanyia uchunguzi wa kina dhihaka hiyo.

“Kuanzia hapo tulimsikia mwenzetu huyu daima akilalamika kuwa mkwe si mwaminifu eti alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamume mwingine hivyo aliapa ‘kumshughulikia’ ipasavyo ili wote wamkose,” alidai mmoja wa wavuvi hao.

Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda, chanzo cha mauaji hayo ya kikatili ni wivu wa kimapenzi na kwamba Ales alifariki dunia muda mfupi baadaye kutokana na kuvuja damu nyingi. Kamanda Mwaruanda alisema mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani.

Jijini Dar es Salaam, Fatuma Selemani (21) mkazi wa Kinondoni Mkwajuni, amemchoma kisu mchumba wake, Selemani Ramadhani (24) mkazi wa Magomeni Somanga, na kufariki dunia akipelekwa hospitali.

Mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo juzi saa saba mchana kwa sababu za wivu wa kimapenzi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Charles Kenyela, Fatuma alimchoma kisu Ramadhani na kukimbilia kwa kaka yake aitwaye, Omary Matimbwa na kumwambia amemchoma kisu kifuani mchumba wake na anatoka damu kama maji.

Katika tukio jingine, Erasto Chalamila anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 30 hadi 40, mlinzi wa Kampuni ya Ultimate Security, mkazi wa Kinondoni Hananasif, amekutwa amekufa ndani ya chumba chake na mwili wake hauna jeraha lolote huku ukiwa umevimba ukitokwa na damu pia ukiwa na harufu kali.

Imeandikwa na Peti Siyame, Sumbawanga na Abdallah Selemani wa Polisi (OUT).

0 comments:

Post a Comment