Saturday, October 20, 2012

Inaelezwa kuwa katika uchaguzi huo, Sophia Simba ametetea kiti chake cha uongozi cha Uenyekiti wa UWT.
Picture
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT, wakiwasili mjini Dodoma kwa uchaguzi unaofanyika Jumamosi Oktoba 20, 2012 (picha, maelezo: K-VIS blog)
Picture
Makamu wa Rais, Dkt. Ali Mohammed Shein, (Kulia), Makamu wa Mwenyekiti wa CCM, (Bara), Pius Mekwa, (Kushoto), na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake, UWT, Sophia Simba, mwanzoni mwa kikao cha uchaguzi cha Jumuiya hiyo, mjini Dodoma, Jumamosi Oktoba 20, 2012
Picture
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM, (UWT), ambaye anamaliza muda wake, Sophia Simba, akiingia ukumbi wa Mipango tayari kwa uchaguzi mkuu wa Jumuiya hiyo mjini Dodoma, Jumamosi Oktoba 20, 2012
Picture
Shy-Rose Bhanji, (Kulia), akionyesha uso wa hasira huku akitulizwa na mjumbe mwenzake, kufuatia tafrani kati yake na mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania UWT), Sophia Simba
Picture
Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, (Aliyekaa), akitulizwa hasira na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwkezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu, wakati wa kikao cha uchaguzi mkuu wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM, UWT, kwenye ukumbi wa chuo cha Mipango Dodoma Jumamosi Oktoba 20, 2012. Taarifa zinasema, mbunge huyo alipandwa na hasira kufuatia majibu yaliyoelekea ya kudhalilisha kutoka kwa mwenyekiti anayemaliza muda wake wa jumuiya hiyo, Sophia Simba, wakati akijinadi na kuulizwa maswali na wajumbe kabla ya uchaguzi kuanza. Sophia Simba ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela

0 comments:

Post a Comment