Saturday, October 20, 2012

JWTZ v/s Polisi: 

Nimefahamishwa kuwa, askari walioavalia sare za  JWTZ walishuka kwenye lori lao na ‘kumlabua’ askari aliyekuwa akiongoza magari kwenye eneo la Ubungo, Dar es Salaam kwa kuwachelewesha kwenye foleni kwa muda mrefu.

Taarifa kutoka chanzo kingine cha habari zikaongeza kusema kuwa Wanajeshi waliohusika ‘kulabua’ walikamatwa baadaye katika eneo la Ilala na sasa wapo rumande.

Jaribio la kupora silaha:

Kwa mujibu wa GPL, mtu mmoja anaedaiwa kuwa ni jambazi  wakiwa na wenzake waliingia katika kambi ya JWTZ 511 KJ bohari kuu ya kijeshi iliyopo Gongo-la-Mboto  jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupora silaha. Kulizuka purukushani baina ya majambazi hayo, askari waliokuwa ulinzi ndani ya kambi hiyo na raia, purukushani ambayo ilimtoa uhai jambazi mmoja.


0 comments:

Post a Comment