Wednesday, October 3, 2012

Basi la abiria la kampuni ya Dar Express limepata ajali ya kuungua na kuteketea kwa moto leo asubuhi katika eneo la Segera kwenye njia panda ya Dar es Salaam-Arusha-Tanga.

Basi hilo lilikuwa likitokea Arusha kuelekea Dar es Salaam likiwa na abiria sitini na tano.

Imeripotiwa kuwa hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa au kupoteza uhai katika ajali hiyo isipokuwa mizigo yote ambayo iliteketea.

Basi hilo lilikuwa na wanafunzi. Askari usalama wa barabarani aliyekuwa zamu katika eneo hilo aliona moshi ukitoka na mara moja akawaamuru abiria wote kushuka. Muda mfupi baadaye gari hilo lilishika moto. Gari la zimamoto kutoka Korogwe lilikuwa likitarajiwa kufika katika eneo hilo kutoa msaada wa kudhibiti moto huo.

---
Picha na maelezo: Samweli Mikuza via blogu ya HabariMseto na tweet ya ITV Tanzania
Picture
(picha hii moja, ni kutoka kwenye blogu ya TangaYetu)
Picture
Basi la Dar Express baada ya kuteketea kwa kuungua moto (picha hii moja imepatikana via Michuzi blog)

0 comments:

Post a Comment