Friday, September 14, 2012

Warembo wa Redd's Miss Temeke, wakiwa mazoezini katika Club ya TCC Chang'ombe, jijini Dar.
Na Mwandishi Wetu
NDANI ya Kambi ya Miss Temeke 2012 kuna moto, imearifiwa kwamba chokochoko zimeanza miongoni mwa warembo 15 wanaowania taji hilo.
Chanzo chetu kimeeleza kuwa chokochoko hizo ni tabia ya warembo kutofautiana hapa na pale, huku sababu ikiwa ni hofu iliyotanda miongoni mwao.
“Kusema ukweli, kwa wakati huu tunajitahidi sana kuhakikisha usalama unakuwepo. Tumeshapokea malalamiko ya huyu akimtuhumu yule kumsema au kumjibu vibaya, hizi tunaziangalia kama chokochoko zinazotokana na hofu.
 
“Kwa kweli warembo wana kila sababu ya kuhofiana wao kwa wao. Unajua kambi ya mwaka huu imebeba warembo wakali watupu, kila aliyeshiriki ana kigezo cha kubeba taji, sasa hapo watashindwa kuogopana?” kilihoji chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina.
Warembo 15 Miss Temeke 2012, hivi sasa wanaendelea na kambi yao kwenye Club ya TCC Chang’ombe tayari wa kinyang’anyiro cha kanda hiyo, kumrithi mrembo Husna Twalib, aliyeshinda mwaka jana.Warembo hao ambao wameanza programu ya shoo tangu wiki iliyopita, chini ya ukufunzi wa Dickson Daud kutoka Kikundi cha THT, wanatoka katika vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang’ombe.

0 comments:

Post a Comment