Saturday, September 15, 2012

SINGIDA, TANZANIA
Polisi watatu wa kike wamefariki dunia papo hapo baada ya gari walilokuwemo wakisafirisha maiti ya polisi mwenzao kupinduka jana asubuhi mkoani Singida.

Polisi waliofariki wametajwa kuwa ni SRosemary Nyabuzuki, Rehema Juma na Nyamwenda Juma

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa amesema kuwa polisi hao wakiwa na wanzao wanane walikuwa wakisafiri kwa gari la polisi  lenye namba PT 1149 wakitokea Morogoro mjini, wakisafirisha mwili wa polisi Regu Kamamo kwenda mkoani Mara.

Sinzumwa amesema ajali hiyo imetokea karibu na kambi ya Wachina, eneo la kijiji cha Manguanjuki, leo saa 5.30 asubuhi, kwa gari kupinduka kutokana na sababu ambayo haijajulikana.

Alisema majeruhi wanane  wa ajali hiyo wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida, na hali zao zinaendelea vizuri.

0 comments:

Post a Comment