Saturday, September 15, 2012

BONDIA David Haye amemwambia Klitschko kuwa hana haki ya kuhofia kutetea ubingwa wake baada ya kushinda pambano lake la jumamosi lilifanyika mjini Moscow,Urusi,dhidi ya bondia wa Syria, Manuel Charr.

Bondia wa Uingereza , Haye ana hamu ya kutwangana na bingwa wa wa Dunia wa WBC, Vitali, ambaye jumamosi alimtwanga ka TKO, Charr katika raundi ya nne.


Haye alisema ' Nilisikitishwa na kiwango kilicho oneshwa na Vital .

Asingeweza kusimama katika raundi sita zilizobakia kama angepigana na mimi. Upiganaji wake ulikuwa mbaya sana .

Anatakiwa kuwa na hofu Klitschko katika pambano hilo alitawala katika raundi zote nne na kuweza kushinda pambano lake la 11 la kutetea ubingwa wake akimwangusha Charr katika raundi ya nne baada ya kumtwanga ngumi ya kichwa.

Charr,mwenye miaka 27 , alichanika juu ya jicho na kusababisha kutokwa na damu nyingi, kitu ambacho kilimfanya muhamuzi kumaliza mpambano huo.


Haye, mwenye miaka 31 aliwahi kutwangwa na mdogo wa Vitali, Wladimir mwaka jana , ambapo alitangaza kustaafu ngumi kabla ya kurejea ulingoni na kumdunda Derek Chisora.


Lakini Vitali, mwenye miaka 41, anasema atastaafu kama akishinda Ubunge katika uchaguzi nchini Ukraine Mwezi ujao

0 comments:

Post a Comment