Tuesday, July 3, 2012

Rais Jakaya Kikwete.
MBUNGE wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba amesema kuwa Rais Jakaya Kikwete ni lazima awe refa wa pambano la wabunge wapenzi wa Simba na Yanga litakalopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Julai 7, mwaka huu.
Kauli ya Nchemba aliyoitoa juzi kwa mwandishi wetu inapingana na ile ya Mbunge wa Kigoma Mashariki, Zitto Kabwe ambaye ni mchezaji wa wabunge wa Simba aliyesema kuwa Rais Kikwete hafai kuwa refa wa pambano hilo kwa kuwa ni shabiki mzuri wa Yanga na anaamini kuwa atawapendelea wabunge wa timu anayoishabikia.

0 comments:

Post a Comment