Tuesday, July 3, 2012

 
Ni vizuri sana kwako kuweza kujua aina ya ngozi yako maana itasidia wewe uweze kuitunza ngozi yako vizuri.Vile vile itakusaidi katika kujua ni vipodozi vya aina gani utumie kutokana na ngozi yako. Hakuna ngozi mbili ambazo zinafanana exactly ila zinatofautiana ambapo inawezekana ngozi yako ikawa ni Ngozi Kavu, Ngozi ya Kawaida, Ngozi ya mafuta na ngozi mchanganyiko yaani combine skin. 
 
Ili kujua ngozi yako ni ya aina gani osha uso wako kwa kutumia sabuni ya kusafishia uso then baada ya dakika 30 chukua tishu na futa sehemu ya paji lako la uso, kwenye pua, kidevu na mashavu. 
 
Kama tishu hiyo haitaonyesha kuwana mafuta baada ya kufuta basi ngozi yako itakua ni aina ya ngozi kavu. 
 
Ngozi kavu huwa inaonekana rough na hukabiliwana mistari na wrinkles lakini kama ngozi yako kuna sehemu nyingine inakua kavu sehemu nyingine inakua na mafuta basi ngozi yako itakua ni ngozi mchanganyiko. 
Ngozi ya kawaida au Normal skin huwa inaonekana laini na ngozi hii ya mafuta ukiigusa unayahisi mafuta na huwa inang`aa. Ngozi hii ya mafuta huwa inakabiliwa sana na blackheads na pimples/chunusi na kwa kuwa ngozi hii ni sensitive inahitaji special care na umakini na vipodozi unavyopaka kwenye uso wako. 
 
Kwa watu wenye ngozi sensitive kama hii ni lazima kutumia misaada ya ushauri kwa wataalamu wa ngozi ili kulinda ngozi zao kupata mzio/allergic. Ni lazima mara kwa mara uwe na utaratibu maalum wa kuihudumia ngozi yako kulingana na mahitaji ya ngozi yako na huenda ikachukua muda mrefu kwa ngozi yako kurudia hali ya kawaida kuweza kuondokana na hili tatizo.

1 comments: