Tuesday, July 10, 2012


Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Singida na mmiliki wa kiwanda cha usindikaji wa mafuta ya alizeti Hussein Nagi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya CCM mkoa kutoa baraka kwa amri ya mkuu wa mkoa kupiga marufuku kwa wafanyabiashara binafsi kununua alizeti moja kwa moja kutoka kwa wakulima. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Waziri katika ofisi ya rais wa uwekezaji na uwezeshwaji kiuchumi Dk. Mary Nagu (wa kwanza kushoto) akijadili jambo na mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone nje ya ofisi ya CCM mkoa wa Singida. Katikati ni katibu mwenezi wa CCM manispaa ya Singida na msaidizi wa mbunge wa jimbo la Singida mjini Hussein Mazala. Dk. Nagu alikuwa mkoani Singida baada ya kutumwa na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pind kwenda kupata taarifa sahihi juu ya amri ya kupiga marufuku wafanyabiasha binafsi kununua alizeti moja kwa moja kutoka kwa wakulima.
Waziri katika ofisi ya rais uwekezaji na uwezeshwaji kiuchumi Dk. Mary Nagu akibadilishana mawazo na katibu msaidizi wa CCM bara na mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki John Chiligati (katikati)na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Joramu Allute (wa kwanza kushoto) nje ya ofisi ya CCM mkoa wa Singida. 
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone akisoma tamko lilolotolewa na CCM mkoa wa Singida kuunga mkono amri yake (Dk.Kone) ya kupiga marufuku wafanyabiashara binafsi kununua alizeti moja kwa moja kutoka kwa wakulima.
Na Nathaniel Limu.
Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida kimebariki amri halali iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone ya kupiga marufuku wafanyabiashara binafsi kununua alizeti moja kwa moja kutoka kwa mkulima.
Baraka hizo zilmetolewa na chama hicho tawala kwenye kikao chake cha halmashauri kuu kilichofanyika mjini Singida.
Kwenye tamko la chama hicho pamoja na mambo mengine, kumedai kubaini kwamba amri hiyo halali, haikueleweka vizuri kwa wananchi na kuagiza elimu ya kutosha kuhusu amri hiyo, itolewe ili lengo la amri hiyo liweze kufikiwa.
Aidha katika tamko hilo, kimesema kuwa amri hiyo haikukataza mtu au kikundi cho chote kununua zao la alizeti, isipokuwa imeelekeza kwamba ni vyama vya msingi vya ushirika ndivyo vitakavyonunua moja kwa moja kutoka kwa wakulima na kisha kuwauzia wafanyabiashara binafsi.
Tamko hilo limesomwa na mkuu wa Singida Dk.Kone, alieagiza kwamba pamoja na vyama vya ushirika kuwepo, kuanzishwe magulio katika maeneo mbalimbali ambayo wakulima wa alizeti watauza kwa watu mbalimbali kwa kufuata bei elekezi.
Akifafanua zaidi Dk.Kone amesema hivi sasa ameteua kamati ambayo itajikita katika kuhakiki uwepo na uwajibikaji wa vyama vya msindi vya ushirika.
Wakati huo huo CCM mkoa wa Singida, imeagiza mamlaka zinazohusika zichukue hatua stahiki za kuanzisha bodi ya zao la alizeti mapema iwezekanavyo.

0 comments:

Post a Comment